Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez akizungumza wakati akizindua Malengo Endelevu 17 ya Maendeleo nchini (SDG’s) Tanzania katika shule ya Uhuru mchanganyiko, katika hafla ambayo pia benki ya Standard Chartered Tanzania ilishiriki na kugawa vitu mbalimbali kwa ajili ya wanafunzi wa shule hiyo. Picha na Zainul Mzige
----
Na Mwandishi wetu
Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez, amesema uondoaji umaskini nchini unawezekana kwa ushirikiano kati ya wadau mbalimbali wa maendeleo.
Kauli hiyo ameitoa mwishoni mwa wiki wakati akizindua Malengo Endelevu 17 ya Maendeleo nchini (SDG’s) Tanzania katika shule ya Uhuru mchanganyiko, katika hafla ambayo pia benki ya Standard Chartered ilishiriki na kugawa vitu mbalimbali kwa ajili ya wanafunzi wa shule hiyo.
Katika hafla hiyo ambayo ilitengenezwa mahususi kuanzisha utekelezaji wa Malengo Endelevu (SDG’s) yakiwemo ya elimu, afya na mazingira Standard walipeleka miti 150 ya kupanda, kompyuta na pia kutumia muda kuangalia afya za wanafunzi.
Alisema katika kukabiliana na umaskini kwa kuangalia Maendeleo Endelevu hakuna kitu kigumu ukilinganisha na ugumu wa mwanafunzi asiyeona kujifunza kwa kupitia vitabu vya nukta nundu na asiyesikia kuwasiliana na mtu mwingine lakini pamoja na ugumu huo watoto hao wanaweza.
Alisema kwa ushirikiano wa wadau kama walivyofanya wao na benki ya Standard Chartered Tanzania anaamini kwamba maendeleo yatafikiwa na Tanzania itafanikiwa kuzika umaskini ifikapo mwaka 2030.
Alisema kutiwa saini kwa Malengo Endelevu na viongozi wa nchi 190 kumeonesha wazi nia ya seriakli mbalimbali duniani kushughulikia umaskini na kuuzika kwa kutekeleza malengo hayo endelevu.
Mwakilishi wa Mkurugenzi wa Benki ya Standard Chartered Tanzania, Charles Katongole akitoa salamu za Mkurugenzi wake ambapo benki hiyo imeahidi kushiriki kikamilifu katika kuhakikisha utekelezaji wa malengo mapya ya Maendeleo Endelevu (SDG's) yanafanikiwa nchini Tanzania. Kushoto ni Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez, Mtaalam wa Mahusiano na Mawasiliano wa Umoja wa Mataifa (UN) Tanzania Hoyce Temu (kulia) pamoja na Mkuu wa Mahusiano wa benki ya Standard Chartered Tanzania, Juanita Mramba (wa pili kulia).
Naye Mwakilishi wa Mkurugenzi wa Benki ya Standard Chartered Tanzania, Charles Katongole, alisema kwamba ni lengo la benki hiyo ni kurejesha faida kwa jamii kupitia miradi yake mbalimbali na kwamba kusaidia shule hiyo ya Uhuru mchanganyiko iliyoanzishwa 01-01-1921 awali ikiitwa Government African secondary school kabla ya kuhamishiwa Mzumbe Morogoro 01-01-1953 na kubadilishwa jina kuwa Kichwele African boys middle school ikiwa na madarasa ya V-VII, ni sehemu ya kurejesha faida kwa jamii.
Alisema ni lengo la benki hiyo kwa mwaka huu kuwezesha kupatikana kwa dola za Marekani milioni 5 kusaidia mambo mbalimbali ya watoto kwa mwaka huu kwa nchi za Afrika mashariki huku Tanzania pekee watoto milioni 10 wakifikiwa.
Benki hiyo yenye matawi Dar es salaam, Mwanza na Arusha katika miradi yake ya afya, vijana na elimu wamekusudia kushirikiana na Umoja wa Mataifa kutekeleza malengo mbalimbali endelevu ikiamini kwamba jamii ikiboreshwa itakuwa katika mfumo mzuri wa maendeleo na kupiga vita umaskini.
Malengo ya SDG’s yamepangwa kutekelezwa katika kipindi cha miaka 15.
Mwalimu Mkuu wa Shule ya msingi Uhuru mchangayiko, Anna Mshana akitoa risala fupi ya shule yake sambamba na changamoto zinazoikabili shule yake kwa ugeni huo kutoka Umoja wa Mataifa na Benki ya Standard Chartered Tanzania.
Mwalimu Mkuu wa shule hiyo Anna Mshana alisema shule hiyo ambayo ilianzisha kitengo cha wanafunzi wasioona 1962 na kubadilishwa kuwa Shule ya msingi Uhuru mchanganyiko mwaka 1964, inakabiliwa na changamoto mbalimbali.
Miongoni mwa matatizo ni miundombinu ya shule hiyo isiyokidhi mahitaji halisi, ukosefu wa ukuta, mashine za kufundishia watoto wasioona, upungufu wa mabweni, magodoro, vitanda na gari la kuwakimbiza hospitalini inapotokea dharura.
Alisema ingawa kuna taasisi hutoa msaada wa gari na matibabu kwa watoto mchana, lakini nyakati za usiku kukitokea dhararu inabidi shule igharamie ingawaje wakati mwingine hatuna fedha inakuwa ni changamoto kwetu.
Alisema Shule ya msingi Uhuru mchanganyiko yenye kutoa elimu jumuishi ina vitengo vya ufundi seremala (1975) wanafunzi wenye mahitaji maalumu ulemavu wa akili (1984) na viziwi na wasioona (Deafblidn) kilichoanzishwa mwaka 1994.
Wanafunzi ambao ni viziwi nao walipata fursa ya kuja kila kinachoendelea kutoka kwa mkalimani wao.
Mkuu wa Mahusiano wa benki ya Standard Chartered Tanzania, Juanita Mramba akitangaza wanafunzi 17 ambao walishiriki shindano la kuhifadhi malengo mapya ya Maendeleo Endelevu (SDG's) wakati wa kukabidhi zawadi kwa wanafunzi hao wa shule ya Uhuru mchanganyiko.
Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez akikabidhi zawadi zilizotolewa na Benki ya Standard Chartered Tanzania kwa wanafunzi hao, sambamba na Mwakilishi wa Mkurugenzi wa Benki ya Standard Chartered Tanzania, Charles Katongole.
Mwakilishi wa Mkurugenzi wa Benki ya Standard Chartered Tanzania, Charles Katongole akimkabidhi Mwalimu Mkuu wa Shule ya msingi Uhuru Mchanganyiko, Anna Mshana (wa pili kushoto) moja kati ya kompyuta tano zilizolotolewa na Benki hiyo ikiwa ni kama ishara ya utekelezaji wa lengo namba nne “Quality Education” wakati wa uzinduzi wa Malengo mapya ya Maendeleo Endelevu (SDG’s) uliofanywa na Benki ya Standard Chartered Tanzania kwa kushirikiana na Umoja wa Mataifa katika shule ya msingi Uhuru mchanganyiko jijini Dar mwishoni mwa wiki. Kulia ni Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez na kushoto ni Mjumbe wa Bodi ya Shule ya msingi Uhuru Mchanganyiko, Bw. Abubakar Mwambungu wakishuhudia tukio hilo.
Kompyuta tano zilizotolewa na Benki ya Standard Chartered Tanzania kwa shule ya Uhuru mchanganyiko.
Mwakilishi wa Mkurugenzi wa Benki ya Standard Chartered Tanzania, Charles Katongole (wa tatu kushoto), Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez (katikati), Mwalimu Mkuu wa Shule ya msingi Uhuru Mchangayiko, Anna Mshana (wa pili kushoto), Mjumbe wa bodi ya kamati ya Shule ya msingi Uhuru Mchanganyiko, Abubakari Mwambungu (kushoto) pamoja na baadhi ya wafanyakazi wa Benki ya Standard Chartered Tanzania katika picha ya pamoja huku wakiwa wameshikilia miche ya miti mbalimbali ikiwemo ya matunda ambapo zaidi ya miche 150 ya miti ilipandwa kuzunguka mazingira ya shule hiyo kulinda mazingira ikiwa ni ishara kwa vitendo ya utekelezaji wa lengo namba 13 "Climate Action" kati ya Malengo 17 mapya ya Maendeleo Endelevu (SDG’s) nchini Tanzania.
Pichani juu na chini baadhi ya wanafunzi na walimu wa shule ya msingi Uhuru mchanganyiko waliohudhuria uzinduzi huo.
Mwakilishi wa Mkurugenzi wa Benki ya Standard Chartered Tanzania, Charles Katongole sambamba na Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez wakishiriki zoezi la upandaji miti kuzunguka maeneo ya shule ya Uhuru mchanganyiko jijini Dar mwishoni mwa wiki.
Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez akishiriki zoezi la upandaji miti sambamba na baadhi ya wanafunzi wa shule Uhuru mchanganyiko.
Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Uhuru Mchangayiko, Anna Mshana akitoa maelezo kwa Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez (aliyeinama) na Mkuu wa Mahusiano wa benki ya Standard Chartered Tanzania, Juanita Mramba (kulia) walipotembelea darasa la awali la watoto wenye ulemavu wa macho (upofu) katika shule hiyo. Nyuma ya Mwalimu Mkuu ni Mjumbe wa Kamati ya Shule ya Msingi Uhuru Mchangayiko, Abubakar Mwambungu.
Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez akicheza na mtoto Fatuma Haji wa darasa la awali katika shule hiyo ambaye ni mlemavu wa macho alipotembelea darasa hilo kabla ya kuzindua wa Malengo mapya ya Maendeleo Endelevu (SDG’s) hafla iliyoandaliwa na Benki ya Standard Chartered Tanzania kwa kushirikiana na Umoja wa Mataifa katika shule ya msingi Uhuru Mchanganyiko jijini Dar mwishoni mwa wiki.
Mwakilishi wa Mkurugenzi wa Benki ya Standard Chartered Tanzania, Charles Katongole, Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez, Mkuu wa Mahusiano wa benki ya Standard Chartered Tanzania, Juanita Mramba pamoja na ujumbe wao katika nyuso za masikitiko walipotembelea darasa la watoto wenye ulamavu wa macho (vipofu) na matatizo ya kutosikia (viziwi) katika shule ya msingi Uhuru mchanganyiko.
Mwakilishi wa Mkurugenzi wa Benki ya Standard Chartered Tanzania, Charles Katongole, Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez, Mkuu wa Mahusiano wa benki ya Standard Chartered Tanzania, Juanita Mramba na ujumbe wao katika picha ya pamoja na wanafunzi ambao ni walemavu wa macho ambao pia ni viziwi katika shule ya msingi Uhuru mchanganyiko.
Walimu wa darasa la watoto wenye ulemavu wa macho ambao ni viziwi wakicheza ngoma na wanafunzi wao.
Maana ya ulemavu wa macho na kuwa kiziwi.
Mkutubi wa maktaba ya shule ya Uhuru mchanganyiko, Masanja akitoa maelezo ya namna mashine za kukuzia maandishi kwa wale wanafunzi wenye uono hafifu katika shule hiyo kwa Mwakilishi wa Mkurugenzi wa Benki ya Standard Chartered Tanzania, Charles Katongole (kushoto) na Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez walipotembelea maktaba hiyo.
Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez akipitia Katiba maalum kwa watu wenye ulemavu wa macho iliyopo kwenye maktaba ya shule hiyo. Kushoto kwake ni Mwakilishi wa Mkurugenzi wa Benki ya Standard Chartered Tanzania, Charles Katongole.
Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez na Ujumbe wa Benki ya Standard Chartered Tanzania ulioongozwa na Mwakilishi wa Mkurugenzi wa Benki ya Standard Chartered Tanzania, Charles Katongole wakitembelea mambweni ya wanafunzi katika shule ya msingi Uhuru Mchanganyiko.
Mwakilishi wa Mkurugenzi wa Benki ya Standard Chartered Tanzania, Charles Katongole, Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez pamoja na baadhi ya wafanyakazi wa Benki ya Standard Chartered Tanzania katika picha ya pamoja na baadhi ya wanafunzi wa shule ya Msingi Uhuru Mchanganyiko.
Mwakilishi wa Mkurugenzi wa Benki ya Standard Chartered Tanzania, Charles Katongole (kulia) na Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez katika picha ya pamoja na wanafunzi wa shule ya msingi Uhuru mchanganyiko Issa Abasi Wenge w darasa la pili (wa pili kushoto) mlemavu wa ngozi na Fatuma Haji (wa pili kulia) wa shule ya awali mwenye ulemavu wa macho.
Mwakilishi wa Mkurugenzi wa Benki ya Standard Chartered Tanzania, Charles Katongole (kulia) na Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez na Mwanafunzi Mariana Alex (Mariana the voice of the SDGs in TZ) wa darasa la tano katika shule ya msingi Uhuru mchanganyiko jijini Dar. #TELLEVERYONE about the #GlobalGoals
Mtaalam wa Mahusiano na Mawasiliano wa Umoja wa Mataifa (UN) Tanzania Hoyce Temu akiserebuka na baadhi ya wanafunzi wa shule ya Uhuru mchangayiko.
Bango lililoorodhesha Malengo 17 mapya ya Maendeleo Endelevu (SDG’s).
Siku ilimazika kwa mechi ya kirafiki baina ya Shule ya msingi Uhuru mchanganyiko na wafanyakazi wa Benki ya Standard Chartered Tanzania katika viwanja vya shule ya sekondari Benjamin Mkapa ambayo ilizinduliwa na Mwakilishi wa Mkurugenzi wa Benki ya Standard Chartered Tanzania, Charles Katongole (kulia) na Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez.
0 comments:
Post a Comment