Mkurugenzi Mtendaji 8020 Fashion na Mentor wa Taasisi ya Manjano Foundation Shamim Mwasha Akitoa Mada kwenye Semina ya Kuwawezesha Wanawake Kuwa Wajasiriamali kupitia Vipodoz Vya Luv Touch Manjano Iliyoandaliwa na Manjano Foundation Kwa Lengo la Kuwajengea Udhubutu Wanawake Kufanya biashara pia namna ya Kujiwekea Akiba na Kutumiza Malengo yao.
Washiriki wa Mafunzo hayo wakisikiliza kwa Makini Mada Mbalimbali zilizokuwa Zikijadiliwa. Mafunzo ya Ujasiriamali kwa Mwanamke wa Kitanzania kwa Kutumia Vipodozi vya LuvTouch Manjano yanaendelea. Mradi huo ulianzishwa kuwejengea Uwezo wanawake Kwenye Ujasiriamali yakisimamiwa na Taasisi ya Manjano Foundation.
Pamoja na mafunzo ya biashara, washiriki hawa watanufaika na utaalamu (Proffessional Makeup Artist).Taasisi ya Manjano Foundation, ambayo imeanzisha jukwaa kwa ajili ya kuandaa miradi na programu ambazo zitamuinua mwanamke wa Kitanzania kwa kumwondolea ugumu wa kipato na ambayo itakuwa ni chachu ya kubadili yale yote yaliyoyazunguka maisha yake. Taasisi hii limekwishazindua mradi wenye kubeba bendera yake, Manjano Dream-Makers, mradi unaokusudia kuzaa kizazi kipya cha wajasiriamali wanawake kwa kutumia kipodozi cha LuvTouch Manjano tu
Mradi huu Uzinduliwa mwezi Mei mwaka huu na Mama Tunu Pinda.
Mafunzo haya yametolewa kwa zaidi ya Wanawake 30 ambapo wengi wao tayari wameshaanza kunuafaika na kipodozi pendwa cha LuvTouch Manjano ambapo wamewezeshwa.
0 comments:
Post a Comment