Vijana wa Tanga wanufaika na mafunzo ya ujasiriamali kupitia Airtel
Fursa
Wafanyabishara wadogo na wa kati zaidi ya 300 waliopo katika wilaya
mbali mbali mkoani Tanga wameongezewa ujuzi wa elimu ya biashara ili
waweze kufanya shughuli zao kwa ufanisi na kuweza kuongezaza kipato chao
na kuchangia pato la taifa.
---
Kampuni ya Airtel
Tanzania, kupitia mpango wake wa “Airtel Fursa Tunakuwezesha” imewapatia
mafunzo ya ujasiriamali vijana wa manispaa ya Tanga kwa lengo la
kuwawezesha kuboresha uendeshaji biashara na kukuza mitaji yao katika
warsha iliyofanyika katika ukumbi wa YDCP uliopo mkoani hapo.
Akifungua
warsha hiyo, meneja mauzo wa Airtel mkoa wa Tanga Aluta Kweka katika
alisema, “lengo letu hasa ni kuwapatia ujuzi vijana wajasiriamali wenye
umri wa kuanzia miaka 18 hadi 24 ili waweze kufanya biashara kwa tija
badala ya kufanya kwa mazoea.
Mafunzo haya tunataraji yataongeza tija ya kibiasha ku kuwawezesha
Vijana hawa kujenga ajira kwa vijana wengine huku wakichochea
upatikanaji wa bidhaa na huduma katika jamii inayowazunguka.
Kufuatia
hatua hiyo baadhi ya wajasiriamali waliohudhuria warsha hiyo
wameishukuru Airtel kwa mchakato huo na wameiomba Airtel kuendelea na
zoezi hilo kwa wafanyabishara nchi nzima ili waweze kufahamu umuhimu wa
kufanya biashara kwa malengo zaidi.
Aisha Mtangi ni mfanyabiashara mdogo anayejihusisha na biashara ya kuuza matunda aliyenufaika na mafunzo hayo ambaye alisema, “kuwa kwa sasa amepata muongozo mzuri utakaokuza biashara zake na kuzifanya kwa weledi mkubwa zaidi”
“Hii ni fursa ya kipekee kwangu kama kijana na ninaishukuru sana Airtel kwa mafunzo yenye manufaa kwangu na vijana wenzangu wa hapa Tanga” Alisema Aisha.
Airtel imejipanga kufikia mikoa 10 kote Tanzania hadi kufikia December mwaka huu. Vijana wa mikoa hii watanufaika na mafunzo ya Ujasiriamali na vitendeakazi kwaajili ya kukuza biashara zao.
0 comments:
Post a Comment