SERIKALI YA UTURUKI YAAHIDI KUISAIDIA TANZANIA KUFANIKISHA ELIMU BURE

 Balozi wa Uturuki nchini Bi.Yasemin Eralp kisalimia na Naibu Spika wa Bunge la Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Tulia Ackson Mwansasu alipomtembelea leo  ofisini kwake.
 Balozi wa Uturuki nchini Bi.Yasemin Eralp akisaini kitabu cha wageni alipotemblea ofisi za Bunge jijini Dar es salaam leo kulia ni Naibu Spika wa Bunge la Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Tulia Ackson Mwansasu .
 Naibu Spika wa Bunge la Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Tulia Ackson Mwansasu akizungumza na Balozi wa Uturuki nchini Bi.Yasemin Eralp alipotembelea ofisi za Bunge Jijini Dar es salaam leo.
 Naibu Spika wa Bunge la Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Tulia Ackson Mwansasu(kulia)  akimuelezea jambo Balozi wa Uturuki nchini Bi.Yasemin Eralp (katikati) na kushoto ni Katibu wa Balozi huyo Bw.Berat Colak
Naibu Spika wa Bunge la Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Tulia Ackson Mwansasu (Kulia) pamoja na maofisa wa Bunge waliokaa kushoto wakizungumza  na Balozi wa Uturuki nchini Bi.Yasemin Eralp (wa pili kulia) na kushoto wa Balozi ni Katibu wa Balozi huyo Bw.Berat Colak Picha zote na Raymond Mushumbusi Maelezo
---
Na Raymond Mushumbusi- Maelezo
Serikali ya Uturuki imeahidi kuisaidia  Serikali ya Tanzania kufanikisha mpango wa utoaji wa elimu bure kwa wanafunzi utakaoanza January mwakani.

Hayo yamezungumzwa leo na Balozi wa Uturuki nchini Bi Yasemin Eralp  alipokuwa akizungumza na Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Tulia Ackson Mwansasu alipomtembelea ofisini kwake.

Balozi yasemin Eralp ameainisha Serikali ya Uturuki imekuwa  ikisaidia  Tanzania katika miradi mbalimbali nakuwa na ushirikiano wa Mabunge  ya nchi hizo mbili ambao umeongeza mahusianio mazuri ya nchi hizo, mbali na ushirikiano wa Bunge ameweka wazi kuwa serikali yake ya Uturuki  inaweza kushirikiana na Serikali ya Tanzania kuwezesha miradi ya maendeleo ikiwemo ujenzi wa barabara, ujenzi wa maktaba za shule,ujenzi wa viwanda na ujenzi wa vituo vya Afya na Hospitali nchini.

“ Katika kuunga  mkono mpango wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika kutoa elimu bure kwa watanzania kuanzia shule ya msingi mpaka sekondari tuko tayari kushirikiana na serikali kwa kutoa msaada  wa vifaa kwa wanafunzi kama vile vitabu, kompyuta na kujenga maktaba katika shule mbalimbali”alisema Balozi Eralp.

Naye Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Tulia Ackson Mwansasu ameishukuru Serikali ya Uturuki kwa kusaidia  Tanzania katika miradi ya kimaendeleo na kuzidi kuomba ushirikiano zaidi toka kwao hasa katika maswala ya Bunge katika nchi hizo.

“ Tunaishukuru Serikali ya Uturuki kwa ushirikiano wao  katika  maswala ya Bunge na kujenga mahusiano mazuri na Tanzania na  hata katika miradi ya maendeleo ya jamii inayofadhiliwa na serikali ya Uturuki na tunaomba tuendeleza mahusiano zaidi katika mahusiano ya mabunge ya nchi hizi mbili ” alisema Dkt Tulia.

Tanzania imekuwa na mahusiano mazuri na Uturuki katika maswala ya Bunge na mwaka 2010 wawakilishi toka Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanznaia chini ya aliyekuwa Spika wa Bunge hilo Mhe. Samwel Sitta walitembelea Bunge la Uturuki kwa mwaliko wa aliyekuwa  Spika wa Bunge la Uturuki wakati huo Mhe.  Mehmet Ali Sahim.
SHARE
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment