WAZAZI, WALEZI WATAKIWA KUWAPELEKA WATOTO SHULE

index 
Mkuu wa Divishen ya Elimu ya msingi Zanzibar Ahmed Abdul Majid akifafanuwa jambo kwa washirikiwa wa mafunzo hayo juu ya Umuhimu wa Elimu ya Maandalizi yaliyofanyika Kituo cha Walimu Kiembesamaki (TC), (kuliya) Mkuu wa Mohamed Othman Dau.
---
Na Majda Kasid –Maelezo Zaznzibar 
Wazazi na Walezi wametakiwa kuwa mstari wa mbele katika kuwapeleka watoto wao waliyofikiwa umri wa miaka minne katika skuli za maandalizi kwa lengo la kuwakuza kielimu.
Hayo yameelezwa na Mkuu wa Divishen ya Elimu ya Msingi Zanzibar Ahmed Abdul Majid wakati alipokuwa akitowa mafunzo kwa wazazi katika Kituo cha Walimu (TC) Kiembe Samaki juu ya umuhimu wa Elimu ya Maandalizi. 
Amesema wazazi na walezi ndio wanao hitajika kufanya bidii kwa kila hali kuhakikisha watoto wanawapa kipaumbele ili kuhakikisha wanapatiwa elimu ya maandalizi na kujiandaa na elimu ya msingi na sekondari.
Amewataka walimu wanaofundisha Wanafunzi kuanzia Elimu ya Maandalizi hadi Elimu ya Sekondari kutowatolesha ada wanafunzi kwani hilo ni agizo lililotolewa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dr. Ali Mohammed Shein.
Alifahamisha kwamba mafunzo hayo yaliyowashirikisha Walimu wa skuli za maandalizi , Walimu wa madrasa , Masheha pamoja na Wazazi yanalengo la kutoa elimu kwa jamii.
Nae Mkuu wa Kituo cha Maendeleo ya awali ya Makuuzi ya watoto (ECD) Muhammed Othman Dau amesema lengo la mafunzo hayo ni kuwaandaa wazazi wa watoto ili waweze kuanzishwa skuli za maandalizi mapema kuwajengea mfumo mzuri wa masomo ya baadae.
Amesema watoto wanapopatiwa elimu ya maandalaizi huwajengea mustakabali mzuri wa maisha ikiwemo upeo wa maadili mema pamoja na kuwa na uwezo wa kubuni mambo ambayo yatawakuza kiakili na kielimu.
Mohammed Othman Dau amesema hadi hivi sasa watoto waliofikia umri wa miaka mine wanaoandikiswa skuli za maandalizi imefikia asilimia 50 na lengo ni kuhakikisha watoto wote wanapelekwa skuli za maandalizi.
Mmoja ya wazazi walioshiriki mafunzo hayo Othman Khamis amesema ni vyema wanafunzi wa maandalizi kupatiwa walimu wa masomo ya dini.
SHARE
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment