Leo Februari 24,2016 ,Chama cha Kimataifa kinachotoa misaada mbalimbali ya Kijamii cha Lions Club International chenye makao yake makuu nchini Marekani kimetoa msaada wa madawati 165 yenye thamani ya shilingi milioni 18 katika shule ya msingi Town na Mwenge zilizopo katika manispaa ya Shinyanga ili kumaliza changamoto ya wanafunzi kukaa chini.
Pichani viongozi wa wilaya ya Shinyanga,wazazi na maafisa kutoka Lions Club International wakiongozwa na Gavana wa Lions Club katika nchi ya Tanzania, Uganda na Sudani ya Kusini bwana Hyderali Gangji wakiwa katika shule ya msingi Town...Madawati hayo 165 yametolewa na Lions Club ya mkoa wa Mwanza.Mwandishi mkuu wa Malunde1 blog,Kadama Malunde ametuletea picha 30 kilichojiri mwanzo hadi mwisho. Gavana wa Lions Club International katika nchi ya Tanzania na Uganda na Sudani ya Kusini Hyderali Gangji alisema wamekuwa wakitoa misaada mbalimbali mkoani Shinyanga ambapo mwaka jana walitoa msaada wa chakula kwa wahanga wa mvua ya Mwakata wilayani Kahama,pia chakula katika kituo cha walemavu wa ngozi cha Buhangija,kutoa madawati katika shule ya msingi Town na Mwenge Miongoni mwa madawati ya chuma 165 yaliyotolewa na Lions Club International katika shule ya msingi Town na Mwenge katika manispaa ya Shinyanga Hapa ni katika shule ya msingi Town katika manispaa ya Shinyanga ,aliyesimama ni mwenyekiti wa bodi ya shule hiyo Said Juma Issa akiwakaribisha viongozi mbalimbali waliofika katika shule wakati wa hafla fupi ya kukabidhi madawati 65 kwa shule hiyo na 100 katika shule ya msingi Mwenge Baadhi ya wanafunzi wa shule ya msingi Town wakiangalia madawati waliyopewa na Lions Club International Kulia ni diwani wa kata ya Shinyanga mjini,ambaye pia ni meya wa manispaa ya Shinyanga Gulam Hafeez Mukadam aliyefanya jitihada za kupatikana kwa madawati katika shule za kata yake,Town na Mwenge.Diwani huyo pia ni mwanachama wa Lions Club International Mwalimu mkuu wa shule ya msingi Town Josephine Mabula akisoma risala kwa mgeni rasmi mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro ambapo alisema shule hiyo yenye wanafunzi 1104 sasa haina uhaba tena wa madawati baada ya kupokea kutoka Lions Club International Kulia ni mkurugenzi wa manispaa ya Shinyanga Lewis Kalinjuna,katikati ni mgeni rasmi,ambaye ni mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro akifuatiwa na gavana wa Lions Club International katika nchi ya Tanzania na Uganda na Sudani ya Kusini Hyderali Gangji Mkurugenzi wa manispaa ya Shinyanga Lewis Kalinjuna akizungumza wakati wa hafla ya kukabidhi madawati,ambapo mbali na kuipongeza Lions Club International kwa kutoa msaada huo,aliwataka madiwani wa manispaa ya Shinyanga kufanya kazi badala ya kukalia maneno maneno kwani kiongozi mzuri anapimwa kwa maendeleo anayowaletea wananchi wake. Mkurugenzi wa manispaa ya Shinyanga Lewis Kalinjuna alisema hivi sasa manispaa hiyo imeanza kutoa shilingi milioni 10 kila mwezi kwa ajili ya kutatua changamoto ya uhaba wa madawati katika shule za manispaa hiyo huku akiwataka wananchi kuendelea kuisaidia serikali kwa michango mbalimbali ili watoto wasome vizuri Gavana wa Lions Club International katika nchi ya Tanzania na Uganda na Sudani ya Kusini Hyderali Gangji akizungumza katika hafla hiyo ambapo alisema wameamua kutoa msaada huo ili kuwaondolea changamoto wanafunzi ya kukaa chini wakati wa masomo ili kuinua kiwango cha elimu hapa nchini ikiwa ni moja ya majukumu yao kusaidiaa jamii na serikali.Alitumia fursa hiyo kuwataka wananchi kujenga moyo wa kutoa kwani serikali pekee haiwezi kumaliza matatizo ya wananchi Wanachama wa Lions Club International mkoa wa Shinyanga wakiwa eneo la tukio,ambao wameahidi kupaka rangi majengo ya shule ya msingi Town Wazazi na walezi wa wanafunzi wakishuhudia kilichokuwa kinaendelea Gavana wa Lions Club International katika nchi ya Tanzania na Uganda na Sudani ya Kusini Hyderali Gangji akijiandaa kukata utepe wakati wa hafla fupi ya kukabidhi madawati 165 kwa shule ya msingi Town na Mwenge zilizopo katika manispaa ya Shinyanga Gavana wa Lions Club International katika nchi ya Tanzania na Uganda na Sudani ya Kusini Hyderali Gangji tayari amekata utepe.... Gavana wa Lions Club International katika nchi ya Tanzania na Uganda na Sudani ya Kusini Hyderali Gangji akishikana mkono na mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro baada kukabidhi madawati 165 Wanafurahia jambo..... Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro akimshukuru Gavana waLions Club International katika nchi ya Tanzania na Uganda na Sudani ya Kusini Hyderali Gangji kwa kutoa msaada wa madawati katika shule za manispaa ya Shinyanga,ambapo alitangaza kujiunga na klabu hiyo ili kuungana na wanachama wengine wa klabu hiyo ambayo imekuwa msaada mkubwa kwa jamii Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro aliishukuru Lions Club International kwa kuisaidia serikali kuchangia shule hizo huku akipongeza jitihada za diwani wa kata hiyo kupigania shule zake kupata msaada huo wa madawati. Matiro alitumia fursa hiyo kuwataka madiwani wa manispaa ya Shinyanga kuiga mfano wa diwani wa kata ya Shinyanga mjini Gulam Hafeez Mukadam ambaye amemaliza tatizo la uhaba wa madawati katika shule za msingi katika kata yake huku akiwataka kufanya kazi ili kuwaletea maendeleo wananchi badala ya kuendekeza siasa na maneno yasiyokuwa na faida kwa wananchi
Aliyesimama ni katibu wa Lions Club ya Shinyanga bwana Sandip Lakhan akizungumza katika hafla hiyo ya kukabidhi madawati.Alisema Lions Club ya mkoa wa Shinyanga imetoa baiskeli kwa mkazi wa Bubiki wilayani Kishapu mkoani Shinyanga Mussa Mipawa,ambaye ni mlemavu wa viungo,iliyotengenezwa na mwanachama wa Klabu hiyo
Mussa Mipawa akiwashukuru wanachama wa Lions Club International kwa kumpa msaada wa baiskeli ya magurudumu matatu
Bwana Mussa Mipawa akishikana mkono na mke wa Gavana wa Lions Club International katika nchi ya Tanzania na Uganda na Sudani ya Kusini Hyderali Gangji
Bwana Mussa Mipawa akiwa katika baiskeli yake
Bwana Mussa Mipawa akiondoka na baiskeli yake-Picha zote na Kadama Malunde-Malunde1 blog Shinyanga.
0 comments:
Post a Comment