Mbunge wa Kilolo Venance Mwamoto akizungumza na wanafunzi wa shule ya Msingi Mhanga ambao wameumbwa na ugonjwa wa kuanguka.
|
Mbunge Mwamoto akiwa na walimu ,wanafunzi na viongozi wa chama na serikali ngazi ya wilaya na mkoa |
|
Mbunge Mwamoto akiwa na walimu wa shule hiyo |
|
Walimu wa shule ya Msingi Mhanga wakiwa katika hali ya hofu
---
WANAFUNZI wa shule ya Msingi Mhanga kata ya Kimara wilaya ya Kilolo wakumbwa na ugonjwa wa kuanguka ovyo kwa zaidi ya miezi sita sasa chanzo kikitajwa kuwa ni vijiti vya ajabu vilivyokutwa mfukoni mwa mwanafunzi mmoja msichana anayesoma darasa la saba .
Mwalimu mkuu wa shule hiyo Zamoyoni Mvella akitoa taarifa ya kuanguka kwa wanafunzi hao mbele ya mbunge wa Kilolo Bw Venance Mwamoto jana alisema kuwa tatizo hilo la wanafunzi kuanguka limekuwa likijitokeza kila siku kwa zaidio ya miezi 6 sasa mfululizo na kuwa idadi ya siku moja kwa wanafunzi kuanguka ni kati ya 8 hadi wanafunzi 16 kwa siku .
Alisema kuwa tatizo hilo lilianza kwa mwanafunzi mmoja wa darasa la saba aliyemaliza mwaka jana ila kwa sasa limeendelea kwa kasi kutoka mtoto mmoja hadi kufikia watoto zaidi ya 15 kwa siku mmoja .
Mkuu huyo alisema kuwa wanafunzi wanaoongoza kuanguka zaidi na wasichana huku wavulana ni mtoto mmoja pekee na kuwa jitihada za uongozi wa shule hiyo ambazo zimefanyika ni pamoja na kutoa taarifa kwa viongozi wa elimu ngazi ya juu ikiwa ni pamoja na kuwaita wazazi wote wa wananfunzi wanaosoma katika shule hiyo wakiwemo viongozi wa dini zote .
Hata hivyo alisema kutokana na kasi hiyo ya wanafunzi kuanguka kuwa juu hofu imezidi kutanda hadi kwa walimu ambao wamekuwa wakihofu kuendelea kufundisha shule hiyo kutokana na ugonjwa huo kutishia maisha yao.
Mwenyekiti wa serikali ya kijiji hicho Bw. Emelius Kihongosi alisema kuwa wanafunzi hao wamekuwa wakianguka kama wagonjwa wa kifafa ila baada ya kufanya tafiti imebainika kuwa wanafunzi hao hawana ugonjwa wa kifafa ila wanasumbuliwa na pepo .
Alisema kuwa chanzo cha tatizo hilo ni mwanafunzi mmoja msichana wa darasa la saba aliyeanguka na baada ya kuzinduka alikuta vijiti mfukoni mwake na baada ya kukuta vijiti hivyo aliwaonyesha wenzake ambao mmoja aliyevitazama pia alianguka na yule aliyetaka kuvichukua vijiti hivyo ili kuvitupa naye pia alianguka pia wakati wanafunzi wakishangaa kwa kutaka kuteketeza vijiti hivyo vya ajabu ndipo alitokea mtu wa ajabu aliyevalia nguo vyeupe na kuchukua vijiti hivyo na kutoweka navyo porini.</td></tr> </tbody></table> |
|
|
0 comments:
Post a Comment