MKURUGENZI WA MTENDAJI WILAYA YA HANANG' AKANUSHA TUHUMA ZA HALMASHAURI YAKE KUTAFUNA FEDHA ZAIDI YA TSH MILINIONI 500

Na woinde shizza wa libeneke la kaskazini blog.
--- 
 MKURUGENZI mtendaji wa halmashauri ya Wilaya ya Hanang’ Mkoani Manyara, Filex Mabula amesema taarifa zilizotolewa kuwa halmashauri hiyo imetumia vibaya zaidi ya sh508.6 milioni fedha za shule na za kusambaza maji vijijini, zilizotolewa na benki ya dunia, siyo za kweli.
Akizungumza na waandisi wa habari jana, Mabula alisema halmashauri hiyo ilitoa sh225.5 milioni kwenye shule za bweni kwa ajili ya chakula kwa mwaka 2013 hadi 2014 sawa na asilimi 281.9 ya fedha zilizoidhinishwa na hazina.
Fedha zetu zinatumika kwa kufuata kanuni na taratibu ndiyo sababu mkuu wa mkoa wetu Joel Bendera alitupongeza Hanang’ kwa kupata hati safi kwa mara ya nne mfululizo kupitia ukaguzi wa ripoti ya CAG,” alisema Mabula.
Alisema sh283.1 milioni zilipelekwa kwenye shule za Katesh, Balang’dalalu, Bassodesh na Gendabi kwa ajili ya ununuzi wa vifaa vya shule na kamati ya fedha iliidhinisha kwa kikao cha Juni 26 mwaka huu na baraza la madiwani Julai 8.  

Alisema vijiji saba vya Getasam, Ng’alda, Gidagharbu, Simbay, Ishponga, Garawja na Galangal, vimepatiwa miradi ya maji kupitia ufadhili wa benki ya dunia na vijiji vya Hirbadaw, Wandela na Dajameda vitanufaika hivi karibuni.  

Wanasiasa msiwakatishe tamaa watendaji bila sababu ya msingi kwa kutumia kipindi hiki cha uchaguzi kuwapotosha wananchi kwani kiongozi bora anapatikana kwa utendaji wa kazi siyo kudanganya jamii,” alisema Mabula.  

Nao, baadhi ya wakazi wa wilaya hiyo walipongeza jitihada zinazofanywa na uongozi wa halmashauri hiyo kupitia mkurugenzi huyo Mabula kwani miradi mingi ya maendeleo imefanikiwa na jamii inanufaika nayo.  

Mkazi wa Katesh, Julius Gidang’ai alisema mara nyingi wanasiasa wamekuwa wakikwamisha miradi mingi ya maendeleo kutokana na kuzusha vitu vya uongo endapo baadhi ya miradi ya maendeleo itakapokuwa haijazifikia kata zao.  

Hivi sasa sisi wananchi wa kata ya Endasak tumeshindwa kuendelea na mradi wetu wa umwagiliaji kule Endagaw baada ya Mabula kusimamia zoezi vizuri lakini wanasiasa wakakwamisha,” alisema Zainab Juma mkazi wa kijiji cha Endagaw.
SHARE
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment