Naibu
waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Hamis
Kigwangala akizungumza mara baada ya kumaliza matembezi ya hisani ya
kuhamasisha uchunguzi wa saratani ya matiti yaliyoandaliwa na Taasisi ya
Saratani ya Hospitali ya Ocean Road jijini Dar es Salaam ambapo huu ni
mwaka wa nne tokea yameanzishwa. Picha na Cathbert Kajuna wa Kajunason Blog.
Mmoja ya wagonjwa ambaye amepona saratani ya matiti akitoa ushuhuda mbele ya wageni.
Askari wakiongoza matembezi ya hisani ya kuhamasisha uchunguzi wa saratani ya matiti yaliyofanyika jijini Dar es Salaam leo.
TAASISI
ya Saratani ya Hospital ya Ocean Road leo imefanya matembezi ya hisani
kwa lengo la Kuhamasisha na kuchangia zaidi ya milioni 120
zinazohitajika kwa ajili ya kununua vifaa tiba vya chemotherapy.
Matembezi
hayo yalianzia Hospitali ya Ocean road na kumalizika hapo hapo huku
wakizunguka moja ya barabara za jiji la Dar es Salaam huku Naibu waziri
wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Hamis Kigwangala
akiwa ni mgeni rasmi.
Matembezi ya hisani ya
kuhamasisha uchunguzi wa saratani ya matiti yaliyoandaliwa na Taasisi ya
Saratani ya Hospitali ya Ocean Road jijini Dar es Salaam
Wananchi waliojitokeza katika mara baada ya kumaliza matembezi ya hisani ya
kuhamasisha uchunguzi wa saratani ya matiti yaliyoandaliwa na Taasisi ya
Saratani ya Hospitali ya Ocean Road jijini Dar es Salaam
0 comments:
Post a Comment