Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Huria (OUT), Profesa Elifas
Bisanda akizungumza kuhusiana na mahafali ya 30 ya chuo hicho yatakayofanyika kesho
(Alhamisi), Biafra jijini Dar es Salaam jana. Picha na Mugishagwe Zablon.
Mugishagwe Zabon, Dar
es Salaam.
Chuo Kikuu Huria Tanzania (OUT), kesho Alhamisi kinatarajiwa
kumtunku udaktari wa heshima Rais mstaafu wa awamu ya nne, Dk. Jakaya Mrisho
Kikwete wakati wa mahafali ya 30 ya chuo hicho yanayotarajiwa kufanyika,
viwanja vya Biafra Kinondoni jijini Dar es Salaam.
Akizungumza wakati wa mkutano na waandishi wa habari leo,
Makamu Mkuu wa chuo hicho, Elifas Bisanda alisema licha ya Rais huyo mstaafu
pia Rais wa Chuo Kikuu cha Chosun cha nchini Korea Kusini, Profesa Chae-Hong
Suh nae atatunukiwa shahada hiyo ya heshima.
“Tutamtunuku Rais huyo wa chuo kikuu Chosan ambaye ambaye
amebobea katika eneo la dawa za binadamu kwani tunafanyanae kazi hapa nchini”
alisema na kuongeza kuwa Kikwete anapewa heshima hiyo kwa chuo kudhamini
mchango wake kimataifa katika kutatua migogoro na ukuzaji uchumi kupitia uwekezaji.
Alisema kiuchumi Kikwete amefanikiwa kwa kiasi kikubwa
kuvutia uwekezaji hali ambayo imechangia Marais wengi wakiwemo wastaafu wa nchi
za Marekani na Ulaya kutembelea nchini akiwemo Rais Barack Obama.
Profesa Bisanda alisema Rais Kikwete amefanyakazi kubwa
kuhakikisha sualuhu inapatikana katika migogoro mbalimbali ukiwemo ule wa baada
ya uchaguzi mkuu nchini Kenya 2007-2008 ambazo zilisababisha vifo vya watu
zaidi ya 1,000.
“Wote tunakumbuka vurugu za baada ya uchaguzi nchini Kenya
ambazo ziisaabisha vifo vya mamia ya raia wasio na hatia na mchango wake jinsi
ulivyowezesha kupatikana kwa utengamano wa kisiasa nchini humo akishirikiana na
Rais wa awamu ya tatu, Mzee Benjamin Mkapa” alisema Bisanda.
Alibainisha kuwa Profesa Chae-Hong Sun wa Chuo Kikuu Chosun
cha nchini Korea ya Kusini ambaye amekuwa na mchango mkubwa katika kusaidia ustawi
wa OUT ambacho pia kina matawi katika nchi mbalimbali za Afrika akiwa amejikita
zaidi katika masuala ya dawa za binadamu.
AIisema licha ya shahada hizo za heshima lakini pia wahitimu
wapatao 69 watatunukiwa shahada za uzamili, uzamivu, stashahada na astashahada
katika mahafali hayo ambayo yaitanguliwa na mengine kama hayo yaliyofanyika, Kampasi
ya Kibaha mkoani Pwani.
Chuo hicho ambacho kina matawi takribani nchi nzima,
kilianzishwa mwaka 1992 hadi hivi sasa kimeishatoa wahitimu zaidi ya 26,763
katika fani na ngazi mbalimbali za kitaaluma.
0 comments:
Post a Comment