CHUO CHA UFUNDI ARUSHA CHATOLEA UFAFANUZI TAARIFA ZA UPOTOSHAJI ZILIZOSAMBAZWA MITANDAONI KUHUSU CHUO HICHO

Uongozi wa Chuo cha Ufundi Arusha (ATC) unautaarifu umma wa Watanzania na Wadau mbalimbali wa Chuo kuwa, hivi karibuni kumekuwepo na taarifa za tuhuma mbalimbali kwenye mitandao ya kijamii dhidi ya Menejimenti ya Chuo, Mkuu wa Chuo, Baadhi ya Watumishi na Mamlaka za Serikali.

Aidha, Uongozi wa Chuo unapenda kukanusha na kueleza Umma kuwa, taarifa hizo hazina chembe zozote za ukweli na zinazushwa na baadhi ya Watu wachache kwa lengo la kupotosha Umma na kwa nia ya kudhoofisha ustawi mzuri wa Chuo.

Vile vile tuhuma hizo zimeeleza kuwepo uonevu kwa baadhi ya Watumishi wa Chuo. Tunapenda Umma ufahamu kuwa, Chuo hakijawahi kumwonea Mtumishi yeyote na maswala yote yanayohusu watumishi hushughulikiwa kwa mujibu wa sheria na kanuni za Utumishi wa Umma na nchi ikiwa ni pamoja na wafanyakazi watatu (03) waliofukuzwa kazi kwa kukiuka sheria hizo na shauri lao liko kwenye Tume ya Usuluhishi na Uamuzi (CMA).

Mwisho tunapenda kuufahamisha Umma kuwa, wakati wowote Chuo kipo tayari kutoa taarifa sahihi kwa Mamlaka zilizoko kisheria.

Ofisi ya Uhusiano Chuo cha Ufundi Arusha (ATC)
Barua pepe: pro@atc.ac.tz, tovuti: www.atc.ac.tz
Imetolewa na:
S.L.P 296, Arusha.
SHARE
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment