MKUU WA MKOA WA DAR ES SALAAM, WAKUU WA WILAYA YA ILALA NA TEMEKE WATEMBELEA SHULE ZA MSINGI.


Bodi ya Wakurugenzi wa Chama cha wamiliki wa Maroli Tanzania(TATOA) na Menejimenti leo iliungana na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam na Wakuu wa Wilaya wa Ilala na Temeke kutembelea shule za Msingi za Majimatitu, Mbande na kisongola ili kujionea hali halisi ya shule hizo na kujua changamoto mbalimbali wanazopitia.

 Hii ni katika kuunga mkono juhudi za Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli katika kuhakikisha kuwa watoto wote wanapewa elimu ya msingi bure. Wanachama wataendelea kupatiwa utaratibu wa namna ya kushiriki kuchangia juhudi hizi.

Afisa Mtendaji Mkuu wa Chama cha wamiliki wa Maroli Tanzania(TATOA) Mhe. Emmanuel J. Kakuyu akiwa katika picha na wanafunzi wa Shule ya Msingi ya Mbande wakati ujumbe mzito wa TATOA ulipotembelea shule kadhaa za Dar es salaam ili kujionea hali halisi ya shule hizo na kujua changamoto mbalimbali wanazopitia na kujua nini cha kusaidia katika kuunga mkono juhudi za Serikali ya awamu ya Tano katika Elimu.
Bodi ya Wakurugenzi wa Chama cha wamiliki wa Maroli Tanzania(TATOA) na Menejimenti leo iliungana na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Said Meck Sadick na Wakuu wa Wilaya wa Ilala, Raimond Mushi na Mkuu wa Wilaya ya Temeke walipotembelea shule za Msingi za Majimatitu, Mbande na kisongola ili kujionea hali halisi ya shule hizo na kujua changamoto mbalimbali wanazopitia.
SHARE
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment