Ni Katibu wa TSD Mkoa wa Singida,Bwana Samweli Ole Saitabau(aliyesimama) akitoa ufafanuzi juu ya upatikanaji wa haki za walimu wa wilaya ya Manyoni ambao bado haapandishwa madaraja yao.
Ni Baadhi ya wanachama wa CWT Wilaya ya Manyoni,Mkoani Singida wakiwa katika mkutano wa pamoja na Naibu Katibu Muu wa CWT,Bwana Ezekiah Oluoch.
---
WALIMU
447 wa shule za msingi na sekondari katika Halmashauri ya wilaya ya Manyoni,Mkoani
Singida hawajapandishwa madaraja yao mbalimbali kutoka mwaka 2014/2015 mpaka
sasa hali ambayo imepunguza ari ya utendaji wao wa kazi za kila siku.
Katibu
wa Chama Cha Walimu (CWT) Wilaya ya Manyoni, Nelea Nyang’uye aliyasema hayo kwenye
taarifa ya kamati ya utendaji ya chama hicho aliyotoa kwa Naibu katibu mkuu
CWT,Ezekiah Oluoch aliyekuwa na ziara ya siku moja wilayani Manyoni iliyolenga
kusikiliza kero pamoja na kuzitafutia ufumbuzi.
Aidha
Nelea alifafanua kwamba kati ya walimu hao,walimu 390 ni walimu wa shule za
msingi na kwamba walimu 276 licha ya kuwa na sifa za kupandishwa madaraja
lakini mpaka wamefikia hatua ya kugota na bila kupandishwa na walimu 114
wanastahili kupandishwa kwa utaratibu wa kawaida.
Kwa
mujibu wa katibu huyo wa CWT, kwa upande wa idara ya elimu sekondari kuna walimu
9 waliogota na walimu 50 wanastahili kupandishwa kwa utaratibu wa kawaida
lakini mamlaka zinazohusika zimeshindwa kushughulikia wilayani hapa.
Kuhusu
malipo ya fedha za likizo,Nyang’uye aliweka bayana kuwa kwa kipindi cha mwezi
disemba,mwaka jana Halmashauri ya wilaya ya Manyoni ilitarajia kupokea shilingi
milioni 30 lakini fedha walizopokea ni shilingi milioni 21 na hivyo kuwa na
upungufu wa shilingi milioni saba.
Hata
hivyo msemaji huyo wa chama alisisitiza kwamba fedha hizo za nauli ya likizo
hupelekwa kidogo sana na kibaya zaidi fedha hizo hupelekwa wakati likizo ikiwa
imeshaanza au inakaribia kwisha,jambo ambalo linapelekea walimu wwenye haki ya
kulipwa kuanza kukopa.
“Nauli
za likizo kuletwa kidogo mno na zinaletwa wakati likizo ikiwa imeanza au
inakaribia kwisha,jambo ambalo linapelekea walimu wenye haki ya kulipwa kuanza kukopa,kwa
mfano nauli ya mwezi disemba,mwaka jana iliyoletwa kwa idara ya elimu ya msingi
ni shilingi 23,000,000/= na idara ya elimu sekondari ni shilingi milioni
saba”alisisitiza katibu huyo wa CWT.
Nyang’uye
hata hivyo alionyesha masikitiko yake kutokana na Tume ya Utumishi wa
Walimu(TSD) wilaya ya Manyoni kushindwa kushughulikia mashauri ya kinidhamu kwa
wakati na hivyo kuchukua muda mrefu sana na kutoa mfano wa shauri moja la
walimu wawili waliosimamishwa kazi tangu mwaka 2013 mpaka sasa hawajuia hatma
yao.
0 comments:
Post a Comment