SERIKALI YA CHINA YATOA MSAADA WA MADAWATI YA TSH MILIONI 20,YAMPONGEZA RAIS DR MAGUFULI KWA UCHAPA MKAZI YAMTAKA WAZIRI WA KILIMO BW NCHEMBA KUSONGA MBELE

mbunge  wa  viti maalum mkoa wa Singida Martha Mlata ambae ni mwenyekiti wa CCM mkoa wa Singida (kulia) akimkabidhi zawadi ya boga kubwa lenye  zaidi ya kilo 7 balozi wa  china nchini Tanzani Dr Lu Yong,ng  baada ya kufanya  ziara wilaya ya Iramba mkoa wa Singida na kutoa msaada wa madawati 400 yenye thamani ya Tsh milioni 20 , kushoto ni waziri wa Kilimo ,mifugo na uvuvi Bw Mwigulu Nchemba ambae ni mbunge wa Iramba pia akiwa ameshika boga la zawadi kwa balozi huyo( picha na matukiodaimaBlog)
Wananchi  wa  kijiji  cha Misigili wakiandaa zawadi kwa ajili ya  balozi wa China alipotembelea  kijiji hicho kutoa msaada wa madawati
Waziri wa Kilimo ,mifugo na uvuvi Bw Mwigulu Nchemba  kulia na mbunge wa viti maalum mkoa wa Singida martha Mlata  wakikabidhi  zawadi ya boga  kubwa  lenye kilo zaidi ya 7 kwa balozi wa China nchini Dr Lu Yong,ng
Waziri wa Kilimo ,mifugo na uvuvi Bw Mwigulu Nchemba  kulia na mbunge wa viti maalum mkoa wa Singida martha Mlata  wakikabidhi  zawadi ya boga  kubwa  lenye kilo zaidi ya 7 kwa balozi wa China nchini Dr Lu Yong,ng
Balozi wa China Nchini Dr Lu Yong,ng akifurahia  zawadi  alizopewa   za  viazi utamu ,maboga na mafuta ya Alizeti kushoto ni waziri wa Kilimo ,Mifugo na uvuvi Bw Mwigulu Nchemba  hapa ni  kijiji cha Misigili wilaya ya Iramba mkoani Singida
Balozi wa China nchine Dr Lu Yong,ng akifurahia zawadi alizopewa ,kulia ni mbunge Martha Mlata
Boga lenye  kilo 7 alilopewa  balozi wa China Iramba Singida
 
Waziri  wa kilimo ,mifugo  na uvuvi Bw Mwigulu Nchemba  akihuka katika ndege aliyoafiria pamoja  na ujumbe wa balozi wa china nchini Dr Lu Yong'ng alipofanya  ziara  jimboni kwake Iramba leo na kukabidhi madawati 400

waziri Nchemba  na mbunge wa viti maalum mkoa wa Singida Martha Mlata wakiungana na balozi wa China nchini Dr Lu Yong,ng kucheza ngoma na  wasanii wa Iramba baada ya kupokelewa ofisi za halmashauri ya Iramba

Sehemu ya madawati iliyotolewa na ubalozi wa China wilaya ya Iramba 

...
Na MatukiodaimaB log ,Iramba

 SERIKALI ya china imepongeza jitihada za  makusudi zenye mwelekeo wa kuwsasskomboa watanzania  zinazo endelea kufanywa na Serikali ya awamu ya tano chini ya Rais Dr John Magufuli  kwa kuwa serikali ya mfano ulimwenguni .

Balozi China nchini Tanzania  Dr Lu Yong,ng  alitoa pongezi hizo jana katika ofisi za Halmashauri ya Iramba wakati akikabidhi madawati 400  yenye thamani ya Tsh milioni 20 kutoka katika ofisi yake na wadau wengine wa maendeleo  kikiwemo chama cha wachimbaji wadogo wa madini nchini ambao waliunga  walichangia madawati 100 kati ya madawati 400 yaliyotolewa na balozi huyo.
Huku balozi huyo  akimpongeza  waziri wa kilimo,mifugo na uvuvi Bw Mwigulu Nchemba kuwa amekuwa ni waziri mchapakazi na kiunganishi sahihi kati ya wa wakulima ,wafugaji na wavuvi kwa serikali na hata nje ya nchi ya Tanzania jambo ambalo limeendelea kuvutia  wengi kuona kuna haja ya kuunga mkono  jitihada za Rais  kupitia wizara ya kilimo katika kuwatumikia wakulima hapa nchini.
Kuwa utendaji kazi wa Rais Dr Magufuli  si tu unawavutia wananchi wa Tanzania pekee bali utendaji kazi wake umekuwa ngunzo na kivutio kwa nchi mbali mbali za Afrika na hata Duniani kwa ujumla nchi nyingi ikiwemo nchi ya China wamekuwa wakivutiwa na utendaji kazi wa serikali ya Tanzania chini ya Rais Dr Magufuli.

Alisema kuwa watanzania walifanya maamuzi mazuri katika uchaguzi mkuu mwaka jana kwa kumchagua mtu sahihi ambae ni Dr Magufuli kuwa Rais na wananchi wa jimbo la Iramba kufanya maamuzi safi ya kumchagua Bw Nchemba kuwa mbunge wao na kuteuliwa na Rais kuwa waziri wa wizara nyeti kwa Taifa ya kilimo.

“Mheshimiwa Mwigulu Nchemba anavyofanya kazi nzuri ya kuimamia wizara yake bado amekuwa hawasahau wananchi wake wa jimbo la Iramba  katika elimu na kilimo pia jambo ambalo mimi nampongeza sana  nimekuwa nikifuatilia vyombo vya habari na kuona jinsi  Nchemba anavyojitahidi kupambana na maendeleo ya wananchi wa jimbo lake pia tutaendelea kuwasaidia maendeleo kupitia kampuni ya China nchini  

Kwani alisema kilimo ni tegemeo kubwa la Taifa  hivyo kuteuliwa kwake kuwa waziri wa wizara hiyo ni ukombozi mkubwa kwa wakulima na jitihada zake zinaonekana na kuifanya serikali kuonekana zaidi nje.
Hata hivyo alisema kuwa kutokana na utendaji mzuri  na uwajibikaji kwa wananchi serikali ya Rais Dr Magufuli imeendelea kupongezwa zaidi ulimwenguni.

Aidha  alisema kuwa ni vema kasi iliyopo nchini ya kuwekeza katika sekta ya elimu kuendelea zaidi ili kupitia elimu kulifanya Taifa la Tanzania  kupaa zaidi katika maendeleo ya  mbali mbali yakiwemo ya Kilimo pia kwani alisema nchini kwake China sekta ambayo imeheshimika zaidi ni  sekta ya elimu na watumishi  wa sekta ya elimu  wakiwemo walimu kwa China ndio ambao huanza kulipwa mishahara yao kabla ya  sekta nyingine zote.
“ Nchini China walimu  wanapata kwanza mishahara ndipo zinafuata sekta nyingine  pia kabla ya  kujenga majengo ya idara  nyingine sisi  tumekuwa  tukianza  kujenga shule bora ,nyumba  za  walimu ndipo  tunanza ujenzi wa majengo ya  sekta nyingine  tumekuwa tukifanya  hivyo kwa  kuamini kuwa elimu ni kila kitu”

Kwa upande  wake waziri Nchemba akimpongeza balozi  huyo kwa msaada  wa madawati na kuonyesha nia ya  kusaidia  wakulima wa Alizeti Iramba  kuwa na viwanda  vya kuchataka alizeti bado  alisema kwa  upande wa wilaya ya Iramba  imekuwa na harambee  kubwa ya  kuona  upungufu wa  madawati  4016   uliopo unafanyiwa kazi kwa nguvu  zote .

Waziri Nchemba  alisema tayari wilaya kupitia pesa  za mfuko wa jimbo na harambee ya kuchangia madawati  imefanikiwa kupata madawati   10400 ambayo kwa  sasa yanaandaliwa na kupitia msaada  huo wa madawati  kutoka ubalozi wa China nchini jumla ya madawati ambayo yamekwisha patikana hadi  sasa  ni 10800 kati ya madawati 4016 yaliyokuwa yanahitajika .

Hivyo  alisema katika  kutekeleza agizo la mkuu wa mkoa wa Singida juu ya ufumbuzi wa  kero ya madawati Halmashauri ya  wilaya ya  Singida imejiwekea mkakati wa kumaliza kero  hiyo ya madawati kwa  muda mfupi  zaidi ili kuona wanafunzi  wote  wanakaa katika madawati wawapo  darasani.

Alisema mbali ya balozi huyo  kufika kukabidhi madawati hayo pia wamelazimika kumpitisha katika tarafa ya Shelui, Ndago  ambako kuna  wakulima  zaidi wa  kilimo cha Alizeti kwa  lengo la  kuwaonyesha  ili waweze  kuwashawishi  wawekezaji kutoka China  kuja kuwekeza viwanda  vya kuchakata Alizeti katika wilaya ya Iramba .

Waziri Nchemba  alisema  iwapo ombi lake  kwa   ubalozi wa China  kuomba  wawekezaji  wa  viwanda kuja mkoani Singida itasaidia  Tanzania ya viwanda kufanikiwa zaidi.



SHARE
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment