WASHIRIKI WA SHINDANO LA AJIRA YANGU BUSINESS PLAN COMPETITION WAASWA KUTUMIA VIZURI FURSA WALIOIPATA

Mkurugenzi Mkuu wa Baraza la uwezeshaji wa wananchi kiuchumi (NEEC), Bang'i  Issa akizungumza wakati wa kufungua masomo ya vijana walioshinda kurishiriki shindano la Ajira yangu Business plan Competition jjini Dar es Salaam leo.
Mkufunzi mkuu wa maswala ya ujasiliamali, Tobias Swai akiwapongeza washindi 50 wa shindano la Ajira Yangu Business Plan Compitition jijini Dar es Salaam leo.
Mwakirishi  kutoka shirika la kazi (ILO), Geras Shirove akizungumza na washindi wa shindano la Ajira yangu jijini Dar es Salaam leo.
Baadhi ya washiriki wa shindano la Ajira yangu waliohudhulia katika shindano hilo wakiwa kwenye mkutano leo jijini Dar es Salaam.

Na Avila Kakingo,Globu ya Jamii.
WASHIRIKI wa shindano la kibiashara  la Ajira yangu Business  plan Competition  wameaswa kutumia  vyema fursa waliyoipata ya kupata mafunzo kwani yanaweza kubadili mitazamo yao ya kimaisha hususani katika masuala ya kujiajiri badala ya kuwa na fikra za kuajiliwa. 

Hayo yamesemwa na Mkurugenzi Mkuu wa Baraza la uwezeshaji wa wananchi kiuchumi (NEEC), Bang'i Issa wakati akizungumza na washirikibwa shindano la Ajira yangu Business plan Competition jiji Daf es Salaam leo. Amesema kuwa watumie fursa hiyo kwani wao ni washindi wa awamu ya kwanza na kuwa kwenye 50 bora kati ya 831. Ni ushindi mmojawapo. 

Bang'i amesema kuwa wazingatie mafunzo watakayoyapata ili wachaguliwe kwe 20 bora na 10 bora.
 Pia amewaasa washiriki wa shindando hilo  kuwatumia vizuri wakufunzi pamoja na mkufunzi mkufunzi mkuu vizuri ili baadae wafanye  umakini vizuri katika kuboresha maandiko yao na kuyawasilisha kwaajili ya mchunjo.

 Nae  mwakilishi  kutoka ILO, Geras Shirove amesema kuwa  amewapongeza washiriki 50 wa kiendelea kushindania shindano hilo kwani washiriki wa shindano hilo walikua 831.
SHARE
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment