ABDULRAHMAN KINANA:SIFA YA KWANZA YA KIONGOZI NI UADILIFU SI KUJENGA BARABARA WALA SHULE

1Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiongozana na Mkuu wa wilaya ya Arumeru Mh. Mwilima Husna Mwilima mara baada ya kuwasili katika kijiji cha Kisongo kwa ajili ya kukagua mradi wa ujenzi wa daraja wakati akiwa katika ziara ya kikazi mkoa wa Arusha akifuatilia na kukagua utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya mwaka 2010.
Akiwa katika jimbo la Arumeru  Magharibi Kinana ameshiriki shughuli mbalimbali za miradi ya maendeleo  na kuzungumza na wananchi jimboni humo akiongozana na Nape Nnauye Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi.
Kinana akiwahutubia maelfu ya wananchi katika mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye viwanja vya Ngaramtoni shule ya msingi, “Sifa ya kwanza ya kiongozi wa ni Uadilifu na sio kujenga barabara wala shule Watu wakuamini kwamba huibi, huwaibii  hiyo ndiyo sifa ya kwanza ya kiongozi”Amesema Kinna.
Ameongeza kwamba kiongozi akiharibu kazi atoke nje serikali hii ni ya chama cha mapinduzi hivyo wana CCM wanatakiwa kuwa wa kwanza kuisafisha  msingoje mtu kutoka nje aisafishe ,  Ninaahidi tutachukua hatua zaidi kuisafisha serikali. 3Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akishieiki kumwaga zege kwa kutumia toroli wakati alipokagua ujenzi wa daraja la Kisongo wilayani Arumeru. 5Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akirudisha toroli mara baada ya kumwaga zege katika ujenzi wa daraja hilo. 7Hili ndilo daraja lenyewe  8 
Nape Nnauye akiongozana na wananchi wa kijiji cha Nduruma wilayani Arumeru wakati alipofika kijiji hapo kusikiliza kero za wananchi. 10Mbunge wa jimbo la Arumeru Magharibi Mh. Gudluck Ole Medeye 11Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akizungumza na wananchi wa kijiji cha Nduruma 12Mbunge wa jimbo la Arumeru Magharibi Mh. Gudluck Ole Medeye akizungumza jambo wakati Abdulrahman Kinana kushoto alipotembelea na kukagua ujenzi wa kituo cha afya cha Manyire kata ya Malangarini , wa kwanza kulia ni Nape Nnauye Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi na wa pili kutoka kulia ni Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Arusha Ole Nangole. 13 
Diwani wa kata ya Mlangarini Mathias Manga  akizungumza jambo wakati Abdulrahman Kinana kushoto alipotembelea na kukagua ujenzi wa kituo cha afya cha Manyire kata ya Malangarini , wa kwanza kulia ni Nape Nnauye Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi na wa pili kutoka kulia ni Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Arusha Ole Nangole.
15 
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akizungumza na wananchi wa kijiji cha Manyire kata ya Mlangarini na kumshukuru diwani wa kata hiyo Bw. Mathias Manga kulia  kwa kujenga kituo hicho16Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akishiriki katika ujenzi wa kituo hicho kwa  kumwaga zege katika nguzo akisaidiana na diwani Mathias Manga. 
17 
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akipata maelezo kutoka kwa Diwania Mathias Manga wakati alipokagua ujenzi wa kituo hicho.18 
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akipata maelezo kutoka kwa Diwania Mathias Manga wakati alipokagua ujenzi wa kituo hicho.19 
Shule ya sekondari ya Sokoni II ambayo Kinana alikagua ujenzi wake pia.20 
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akishiriki ujenzi wa shule ya Sokoni II  wakati alipokagua ujenzi wa shule hiyo.
SHARE
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment