Mrembo wa mkoa wa Tanga 2014/15,Diana Festo akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya walimu na wanafunzi wa Shule ya Msingi Pangani wakati wa hafla fupi ya kukabidhi zawadi hizo.
Mwalimu wa Shule ya Msingi Pangani,akimtambulisha mrembo huyo kwa wanafunzi wa Darasa lake.
MREMBO
wa mkoa wa Tanga 2014/15, Diana Festo ametoa zawadi za vifaa vya shule
kwa wanafunzi wasio jiweza katika shule za msingi Wilayani Pangani,ili
kufanikisha azma yake ya kuwataka wanafunzi kutambua umuhimu wa elimu na
kuweka juhudi na kuzingatia masomo..
Shule
ambazo zilipata nafasi ya kutembelewa na Mrembo huyo na kufanikiwa
kupata vifaa hivyo ni ni shule ya msingi Pangani,Funguni, Mwela na shule
ya msingi Mwembeni ambazo zote zinapatikana katika wilaya hiyo ya
Pangani,huku vifaa vilivyokabidhiwa vikiwa ni Madaftari,Pencel,Rula
pamoja na Kalamu ambazo ndio nyezo kuu za kujifunzia.
Pia
Mrembo huyo alitembelea kituo cha watoto yatima na waishio katika
mazingira magumu chini ya uangalizi wa mawatawa (Sisters) kiitwacho CASA
DELA JOIR (wakoregina wa familia takatifu) kilichopo tanga mjini maeneo
ya Bombo Hospital,ambapo pia aliwapatia watoto walio shule vifaa vya
shule.
0 comments:
Post a Comment