Na MatukiodaimaBLOG
MWENYEKITI wa baraza la Vijana wa Chadema (BAVICHA)
kijiji cha Luana wilaya ya Ludewa mkoani Njombe Bw Kalolo Nkwera
amempongeza mbunge wa jimbo la Ludewa Deo Filikunjombe (CCM) kwa
jitihada zake za uboreshaji wa barabara za wilaya ya Ludewa ikiwemo
barabara ya kijiji hicho yenye urefu wa kilomita 2 aliyoichonga mbunge huyo kwa kushirikiana na wanakijiji kwa gharama ya zaidi ya Tsh milioni 54.
Bw
Nkwera alisema kuwa jitihada zilizofanywa na mbunge Filikunjombe
katika wilaya ya Ludewa ni kubwa na kila mwananchi wa Ludewa na
wasio wa Ludewa ambao wanafika wilayani humo ni mashahidi wa
maendeleo ya sasa ya wilaya hiyo na wao kama wapinzani wanatambua
mchango mkubwa wa mbunge huyo katika maendeleo hivyo hawana sababu ya
kutafuta mbunge zaidi nje ya Filikunjombe.
Mwenyekiti
huyo wa BAVICHA alisema toa kauli hiyo leo wakati akizungumza na
wanahabari baada ya kushirikiana na mbunge huyo na wananchi wengine
katika shughuli ya kimaendeleo ya kuchimba mifereji ya kupitisha
maji kweye barabara hiyo mpya .
"
mimi hapa na baadhi ya wananchi hapo ambao wamekuja kushirikiana
na mbunge Filikunjombe katika uchimbaji wa mifereji ya kupitisha maji
katika barabara hii ni watu wa upinzani kama mimi ni mwenyekiti wa
BAVICHA katika kijiji hiki ila katika masuala ya kimaendeleo mambo ya
itikadi za vyama tunaweka kando na kufanya maendeleo .......hii
barabara tunapita wote hivyo hatuwezi kuwa wapinzani wa maendeleo
yetu"
Bw
Nkwera alisema kwa kazi iliyofanywa na mbunge huyo katika jimbo la
Ludewa kwa kipindi cha miaka 5 ni kubwa zaidi na inaweza imezidi
hata ile ya wabunge waliokaa madarakani zaidi ya miaka 40 bila kufanya
kazi kubwa kama hiyo ya mbunge wa Ludewa.
Hata
hivyo alisema ili Ludewa izidi kusonga mbele zaidi hakuna sababu ya
wana Ludewa kufanya siasa za maeneo mengine za kuvutana kwenye mambo
ya maendeleo kwani kufanya hivyo ni kujikwamisha zaidi katika
maendeleo kama ilivyo kwenye majimbo mengine ambayo wabunge wanafanya
kazi katika mazingira magumu na wafuasi wa chama cha upinzani
hawatakiwi katika shughuli za CCM na wale wa CCM hivyo hivyo japo kwa
Ludewa kwenye mambo ya kimaendeleo ni wananchi wote na vyama
vinawekwa kando.
Mwenyekiti
wa serikali ya kijiji cha Luana Bw David Luoga alisema kuwa
wananchi hao kamwe hawatamsahau mbunge huyo kwani ameweza
kuwaharakishia maendeleo ya kijiji hicho kwa kufikisha umeme na
kuwatengenezea barabara hiyo ya Malatu - Itungi ambayo ilikuwa
haipitiki japo inaelekea katika taasisi mbali mbali kama nyumba za
ibada, soko, Zahanati na shule ila serikali ya wilaya haikuona sababu
ya kuitengeneza hadi wananchi hao walivyoomba kwa mbunge huyo
katika mkutano wao wa hadhara uliofanyika miezi mitatu iliyopita .
Bw
Luoga alisema toka nchi ipate uhuru wake mwaka 1961 kijiji hicho
hawajapata barabara nzuri kama hiyo ambayo ni barabara muhimu ambayo
haikupewa umuhimu wowote na serikali ya wilaya ya Ludewa.
Hivyo
alisea ahsante yao kwa mbunge wao kwa kuwaletea maendeleo ni kuona
wanamchagua kwa kura nyingi zaidi ili kuendelea kuwa mbunge kwa
vipindi vingine 15 ama zaidi na kuwa kipimo chake kilikuwa ni
miaka mitano hii ambayo ameonyeha ufaulu wa zaidi ya asilimia 100
hivyo kama kijiji wananchi wameweza kuchangishana na kupata kiasi cha
Tsh 100,000 kwa ajili ya kwenda kuchukulia fomu muda wa kufanya
hivyo utakapofika.
Kwa
upande wake mbunge Filkunjombe pamoja na kuwapongeza wananchi hao
wakiwemo wale wa Chadema ambao walijitolea kushirikiana nae katika
ujenzi wa barabara hiyo bado alimpongeza mkurugenzi wa kampuni ya
barabara ya Boimanda chini ya mkurugenzi wake Nicholaus Mgaya kwa
kuendelea kuwa mzalendo na wilaya ya Ludewa kwa kujitolea mitambo ya
kuchonga barabara hiyo bila malipo.
Alisema
ni wakandarasi wachache sana wazalendo ambao wanajitolea kwa
wananchi kama hivyo na kuwa kampuni hiyo si tu imekuwa ikijitolea
katika jamii bali ni moja kati ya kampuni za kizalendo ambazo zinafanya
kazi ya ujenzi wa barabara kwa uaminifu mkubwa bila kulipua kama
zilizokampuni nyingine za ukandarasi ambazo hugeuza wilaya hiyo ya
Ludewa ni shamba la bibi kwa kujenga barabara kwa kiwango cha chini ili
mradi wachume pesa.
Mbunge
Filikunjombe aliwataka wananchi hao wa Luana kutunza barabara hiyo
badala ya kuiharibu kwa kupitisha mifugo na kuwa kutengenezwa kwa
barabara hiyo kutapunguza maswali ya wananchi katika mikutano ya
hadhara kwa wananchi hao kila mkutano kutoa kilio cha barabara hiyo
huku akisisitisha kuwa kero zipo nyingi haziwezi kumalizika zote
kwa wakati mmoja japo kwa kuchagua moja moja ipo siku zitamalizika
zote .
"Leo kikao cha bunge kinaendelea bungeni ila nimeona ni vizuri kukimbia mara moja kuja kutatua kero hiyo ya barabara ambayo ilikuwa ikiwatesa wananchi wangu kwanza .....kwani ubunge huu ni wa wananchi hivyo lazima pale ninapoweza kuwasaidia kero zao"
Wakati
huo huo mbunge Filikunjombe amewapongeza wananchi wa Luana kwa
kumchangia kiasi hicho cha pesa za kuchukulia fomu pia kumpongeza
mwenyekiti wa BAVICHA kwa kujitoa kwake katika shughuli za
maendeleo pasipo kutanguliza itikadi za chama chake na kuwataka wana
Ludewa kushikamana katika mambo ya kimaendeleo badala ya kujikita
katika siasa za kupinga maendeleo kama ilivyobaadhi ya majimbo hapa
nchini.
|
0 comments:
Post a Comment