Mwanafunzi wa Shule ya Kimataifa ya Fedha mwaka 11, Khalfan Kikwete (kulia) ambaye alishinda medali ya dhahabu pamoja na mwenzake Seif Yahya Mhata wakizungumza na waandishi wa habari. Mwanafunzi wa Shule ya Kimataifa ya Fedha mwaka 11, Seif Yahya Mhata (kulia) wakizungumza na mmoja wa waandishi wa habari. Mwanafunzi Veronica Samuel Ndomba akielezea mchanganuo wake ulioshinda katika mashindano ya Genius Olympiad kwa wanahabari leo.[/caption]
[caption id="attachment_58800" align="aligncenter" width="619"] Wanafunzi Goodluck Komba (kulia) na Sajjad El-Amin walioshinda na andiko la mradi wa kutengeneza mkaa kwa kutumia makaratasi taka ambao ulishika nafasi ya tatu katika mashindano ya Genius Olympiad wakizungumza na waandishi wa habari. Mwanafunzi Veronica Samuel Ndomba (kushoto) akifanyiwa mahojiano na mmoja wa waandishi wa habari. Mwanafunzi wa Shule za Fedha, Prince Mwemezi Muzamil Katunzi akielezea picha yake ilioshinda katika mashindano ya Genius Olympiad kwa wanahabari leo. Mwanafunzi Veronica Samuel Ndomba akielezea (kulia) katika picha na abendera ya nchi yake mara baada ya ushindi katika mashindano ya Genius Olympiad hivi karibuni. Picha ya Mwanafunzi Prince Mwemezi Muzamil Katunzi aliyoipiga na kushinda katika mashindano ya Genius Olympiad. Kutoka kulia ni mwalimu Metin Er wa Masomo ya Biashara, Fedha International School na Meneja Uhusiano wa Ishik Medical & Education Foundation.
---
WANAFUNZI sita wa Shule za Feza Tanzania wameshinda mashindano ya taaluma kimataifa 'Genius Olympiad' yaliyoshirikisha nchi mbalimbali katika vipengele tofauti na kuzawadiwa medali za dhahabu, shaba pamoja na zawadi mbalimbali.
Wakizungumza na waandishi wa habari leo katika moja ya shule za Feza iliyopo Kawe jijini Dar es Salaam Wanafunzi hao kuelezea ushindi wao wameshauri wanafunzi wengine kupenda kushiriki katika mashindano anuai ya taaluma kwani ni njia ya kuwaongezea maarifa shuleni.
Wanafunzi walioshinda na kupewa medali ni pamoja na Seif Yahya Mhata, Khalfan Jakaya Kikwete, Prince Mwemezi Muzamil Katunzi, Goodluck Komba, Sajjad El-Amin na Veronica Samuel Ndomba.
Akizungumza mwanafunzi wa Shule ya Kimataifa ya Fedha mwaka 11, Khalfan Kikwete ambaye alishinda medali ya dhahabu pamoja na mwenzake Seif Yahya Mhata alisema wazo lao lililoshinda lilikuwa ni la kutengeneza mfumo wa kuhifadhi mawasiliano ya mtu kupitia simu za mkononi (A virtual business cards & New generation business social media, Vcardin) andiko ambalo wameliwasilisha na kushinda wote medali za dhahabu.
Alisema utafiti unaonesha njia ya kutengeneza card za mawasiliano kwa kutumia karatasi kwa wafanyabiashara na wafanyakazi zimekuwa zikileta madhara kimazingira pamoja na kupotea baada ya muda, hivyo wao kubuni mfumo (App) wa kuhifadhi mawasiliano hayo upitia simu za mkononi (iphone) ambao ni bora na unatunza kwa uhakia. Wanafunzi wa Shule za Feza Tanzania walioshinda mashindano ya taaluma kimataifa ya 'Genius Olympiad' katika picha ya pamoja. Wanafunzi wa Shule za Feza Tanzania walioshinda mashindano ya taaluma kimataifa ya 'Genius Olympiad' katika picha ya pamoja na baadhi ya walimu wao. Wanafunzi Goodluck Komba na Sajjad El-Amin.
Mwanafunzi Yahya Mhata ambaye kwa pamoja wamebuni mfumo huo, ameuelezea kuwa ni mzuri na rafiki wa mazingira huku ukiweza kuhifadhi kumbukumbu za mawasiliano kwa uhakika tofauti na ule wa kadi za makaratasi ambao wengi hupoteza kadi hizo na kujikuta wakipoteza mawasiliano muhimu.
Wanafunzi wengine wa Shule za Fedha ambao ni Prince Mwemezi Muzamil Katunzi, Goodluck Komba, Sajjad El-Amin na Veronica Samuel Ndomba ambao kila mmoja ameshinda medali za fedha katika makundi ya ushindani tofauti chini ya usimamizi wa mwalimu Metin Er wa Masomo ya Biashara, Fedha International School walieleza kunufaika na mashindano kitaaluma na upeo.
Mwanafunzi Mwemezi Muzamil Katunzi, ambaye aliwasilisha picha yenye ujumbe wa mazingira na kushinda alisema picha hiyo aliipiga eneo la viwanja vya Tanganyika Packers jijini Dar es Salaam ikielezea namna binadamu wanaathiri mazingira kwa kuchoma moto hovyo na kuleta matatizo mengine duniani.
Kwa upande wao wanafunzi Goodluck Komba na Sajjad El-Amin waliwasilisha andiko la mradi wa kutengeneza mkaa kwa kutumia makaratasi taka ambao ulishika nafasi ya tatu katika mashindano ya Genius Olympiad yaliyofanyika jijini New York.
Mwanafunzi Komba alisema mradi wao ni rafiki wa mazingira na ukitumika utaokoa sehemu kubwa ya uharibifu wa mazingira.
Kwa upande wake msichana pekee aliyeshinda katika mashindano hayo, Veronica Samuel Ndomba alisema andiko lake lilishinda kwenye kipengele cha 'Mazingira Yetu' na aliandika kuonesha namna elimu ya mazingira inaweza kutolewa na kulinda uharibifu mkubwa wa mazingira unaofanywa katika shughuli mbalimbali za binadamu.
Naye msimamizi wa wanafunzi hao, mwalimu Metin Er alisema kundi hilo la wanafunzi mbali na kujijenga kimaarifa kwa wanafunzi hao wameiletea sifa Tanzania kwani kwani mashindano hayo ya kitaaluma yalishirikisha nchi mbalimbali zikiwemo USA, Romania, Nigeria, Tunisia, Holland, Turkmenistan, Kazakhstan and Russia. Shule za Fedha International School zimekuwa zikifanya vizuri kitaaluma kitaifa na kimataifa jambo linaloendeleza umaarufu wa shule hizo kila uchao.
0 comments:
Post a Comment