VETA YAIBUKA MSHINDI WA KWANZA KATIKA ENEO LA UENDELEZAJI UJUZI NA UTOAJI MAFUNZO, SABASABA

Mkurugenzi Mkuu wa VETA, Mhandisi Zebadiah Moshi akionesha cheti cha ushindi wa kwanza wa VETA katika eneo la Uendelezaji Ujuzi na Utoaji Mafunzo katika Maonesho ya 39 Biashara ya Kimataifa (Sabasaba) baada ya kutunukiwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mh. Dk Jakaya Mrisho Kikwete (wa pili kutoka kushoto) kwenye sherehe za ufunguzi tarehe 3 Julai 2015. Wengine kushoto ni Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Biashara Tanzania Mama Jacqueline Maleko na kulia ni Waziri wa Viwanda na Biashara Dk. Abdallah Kigoda.
Washiriki wa VETA katika Maonesho ya 39 Biashara ya Kimataifa (Sabasaba) wakiwa katika picha ya pamoja kushangilia ushindi wa kwanza wa VETA katika eneo la Uendelezaji Ujuzi na Utoaji Mafunzo. Mbele walioketi kwenye viti katikati ni Mkurugenzi Mkuu wa VETA, Mhandisi Zebadiah Moshi, kushoto ni Mkurugenzi wa Mafunzo, Bi. Leah Dotto Lukindo na kulia ni Mwenyekiti wa Banda la VETA katika Maonesho ya Sabasaba Bi. Rehema Binamungu.
SHARE
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment