Mkuu wa wilaya ya Sengerema Mhe Zainab Rajabu Telack akiwahutubia Wananchi waliojitokeza katika Sherehe za uzinduzi wa Mkakati wa Uasajili na kutoa Vyeti vya kuzaliwa bure kwa Watoto wenye Umri chini ya miaka Mitano kwa kifupi (U5BRI) hafla iliyofanyika katika viwanja vya Kituo cha Afya Project wilayani Sengerema.
Mkuu wa wilaya hiyo akimwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhe Magesa Stanslaus Mulongo kama Mgeni rasmi katika Uzinduzi huo ametoa wito kwa wananchi kujitokeza kwa wingi katika kampeni ya siku saba kuanzia Tarehe 30 juni 2015 hadi 6 julai 2015 katika vituo vyote vya Tiba vinavyotoa huduma ya Mama na Mtoto kwenye wilaya zote za Mkoa wa Mwanza.
Tayari Mkakati kama huu ulizinduliwa mwaka 2013 na kutekelezwa katika Wilaya zote za Mkoa wa Mbeya na kuonesha mafanikio makubwa kwani hadi sasa zaidi ya Watoto laki mbili wamesajiliwa na kupatiwa vyeti vya kuzaliwa bure.
Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa RITA Bi Emmy Hudson akiwahutubia Wananchi waliojitokeza katika Sherehe za uzinduzi wa Mkakati wa Uasajili na kutoa Vyeti vya kuzaliwa bure kwa Watoto wenye Umri chini ya miaka Mitano katika viwanja vya Kituo cha Afya Project wilayani Sengerema.
Wafanyakazi wa RITA wakiwa katika picha ya pamoja na mgeni rasmi ambaye ni Mkuu wa Wilaya ya Sengerema Mhe Zainab Rajabu Telack (katikati) walioketi.
0 comments:
Post a Comment