Mkurugenzi wa Global Link Education (GEL) ambao ni Mawakala wa Vyuo Vya Nje ya nchi, Abdulmaliki Mollel akitoa maelezo katika semina ya kuwajengea uwezo wazazi na wanafunzi wanaokwenda kusoma Vyuo Vikuu vya India na China leo katika ofisi zao zilizopo viwanja vya Mwalimu Julias Nyerere Barabara ya Kilwa jijini Dar es Salaam.
Meneja Mkuu wa Global Link Education (GEL) ambao ni Mawakala wa Vyuo Vya Nje ya nchi, David Nsimba akitoa semina ya kuwajengea uwezo wanafunzi wanaokwenda kusoma Vyuo Vikuu vya India na China leo katika ofisi zao zilizopo viwanja vya Mwalimu Julias Nyerere Barabara ya Kilwa jijini Dar es Salaam.
Wanafunzi waliosimama wanakwenda kusoma katika vyuo vya China nao walipata fursa ya kuhuduria semina ya kuwajengea uwezo kuwajengea uwezo wa mazingira katika vyuo hivyo na jinsi ya kuanza safari yao Agosti 21, 2015. Semina hiyo ilifanyika ofisi za GEL zilizopo viwanja vya Mwalimu Julias Nyerere Barabara ya Kilwa jijini Dar es Salaam.
Meneja Mkuu wa Global Link Education (GEL) ambao ni Mawakala wa Vyuo Vya Nje ya nchi, David Nsimba akikabidhi Hati ya Kusafiria (passport) pamoja na visa kwa mmoja ya mwanafunzi wanaokwenda kusoma Chuo Kikuu nchini China, makadhiano hayo yalifanyika leo ofisi za GEL zilizopo viwanja vya Mwalimu Julias Nyerere Barabara ya Kilwa jijini Dar es Salaam.
Sehemu ya wazazi wakiwa na watoto wao wanaotarajia kwenda kusoma Vyuo Vikuu vya nchini India na China wakiwa katika semina ya kuwajengea uwezo iliyofanyika katika ofisi zao zilizopo viwanja vya Mwalimu Julias Nyerere Barabara ya Kilwa jijini Dar es Salaam. (Picha na Emmanuel Massaka, GLOBU YA JAMII)
---
Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii.
Kampuni ya GLOBAL link Education (GEL) ambao ni Mawakala wa Vyuo Vya Nje ya nchi leo imewapa semina zaidi wanafunzi 100 kwa wanaokwenda kusoma katika vyuo vya India na China katika kuwaandaa katika mazingira watakayokutana nayo kuanzia safari hadi kufika katika nchi hizo.
Akizungumza na wazazi pamoja na wanafunzi wanaokwenda kusoma vyuo katika nchi hizo, Mkurugenzi wa Global Link Education, Abdulmaalik Mollel amesema kufanya semina hiyo ni kuwaandaa wanafunzi jinsi ya kwenda kusoma katika vyuo na kuja kuendeleza nchi yao katika teknolojia mbalimbali.
Amesema vyuo wanavyokwenda kusoma wanafunzi ni vyuo vyenye ubora wa elimu na sio majina ya vyuo yote hiyo ni kuandaa vijana katika soko la ajira uwigo mpana wa ndani na nje ya nchi au kujiajiri na kuleta mapinduzi katika nchi.
Mollel amesema kuanzia Septemba hadi Novemba itakuwa ni kusafiri kwa wanafunzi ambao wamepitia Global Link Education kwenda katika vyuo vinavyofanya vizuri na baadhi ya wanafunzi wamefaulu vizuri katika madaraja yanayokubalika katika ajira duniani.
Amesema Global Link Education wako katika utaratibu kuingia mkataba na makampuni mbalimbali kwa ajili ya wanafunzi wanaokwenda nje wakimaliza kuingia moja kwa moja katika soko la ajira ili kuondoa usumbufu kwa wanafunzi.
Mollel amesema hadi kufikia Oktoba wanatakuwa wamepeleka wanafunzi zaidi 600 katika vyuo mbalimbali ambavyo Global Link ni wakala wa vyuo hivyo .
Amesema waliokwenda India hadi sasa wamefikia 170 na bado wanaendelea kwenda na wanafunzi wengine zaidi 100 wanasubiriwa kutokana na kuwa katika Mafunzo ya Jeshi la Kujenga Taifa (JKT).
Aidha amesema kuwa zaidi 100 wamepewa tiketi na visa katika vyuo vya nchi hizo ambayo kazi hiyo inafanywa na Global Link Education kwa kila hatua.
Amewataka wazazi katika kipindi hiki kifupi walete watoto wao kutokana kuwepo kwa nafasi katika vyuo vya India na China kutokana na kuwepo kwa maombi maalum.
Wazazi waliuliza juu ya kuharibikiwa kwa watoto katika vyuo vya nje ambapo Mkurugenzi wa Global Linki Education amesema kuharibikiwa huko kunatokana na wazazi kuwapa fedha nyingi za ziada na kufanya kujiingiza katika michezo michafu.
Mollel amesema wazazi watoe fedha kutokana na hali halisi ya matumizi ya mwanafuzi katika chuo husika au kuweza kuuwasiliana na Global kwa kusahauri jinsi ya kuweza kudhibiti matumizi ya mtoto akiwa chuoni.
Amesema kuwa wanafunzi hao wanakwenda ni watoto hivyo hawana udhibiti wa fedha hivyo lazima wazazi wawajue watoto matumizi yao.
0 comments:
Post a Comment