Mwezeshaji wa mafunzo hayo Bi FORTUNATA MAKAFU akiendelea kutoa mafunzo mbalimbali kwa wanafunzi wa vyuo waliojitokeza katika mafunzo hayo Leo Jijini Dar es salaam.
Kituo cha Msaada wa sheria kwa wanawake na watoto (WILAC) leo wamekutana na wanafunzi wa vyuo mbalimbali nchini Tanzania katika mwendelezo wa utaratibu wa shirika hilo wa kutoa elimu kwa makundi mbalimbali nchini ya kujiandaa na zoezi la uchaguzi mkuu ambao unataraji kufanyika october 25 mwaka huu.
Mafunzo hayo ambayo yanadhaminiwa pia na shirika la kimataifa la OXFARM yana lengo la kuhakikisha kuwa makundi mbalimbali yakiwemo walemavu,kina mama,wanafunzi na makundi mengine wanatambua umuhimu na mchango wao katika zoezi la kupiga kura ikiwa ni pamoja na kuwahamasisha kujitokeza kwa wingi kupiga kura.
Katika mafunzo hayo ambayo mtandao huu ulipata nafasi ya kuhudhuria yalijikita zaidi kuwasaidia wanafunzi hao ambao ni wa vyuo mbalimbali nchini kuelewa jinsi gani ya kufanya uchaguzi wa mwaka huu kuwa ni uchaguzi utakaomalizika kwa amani kwa kufwata sheria,kanuni,na taratibu mbalimbali zilizowekwa na vyombo husika ili nchi ya Tanzania iendelee kuwa na amani ya kudumu mara baada ya uchaguzi huo.
Baadhi ya wanafuzi ambao wamepata nafasi ya kuzungumza na mtandao huu nje ya mafunzo hayo wamesema kuwa mafunzo hayo yamewasaidia sana hususani kujitambua na kutambua nini wajibu wao wakati wa uchaguzi mkuu na nini wazingatie ili kupata viongozi ambao ni bora.
Baadhi ya mambo ambayo wanafunzi hao wamekiri kuwa bado ni changamoto kwa wanafunzi wengi kuelekea uchaguzi mkuu ni pamoja na kuwepo kwa idadi kubwa ya wanafunzi ambao wapo hatarini kuikosa haki hiyo ya kupiga kura kutokana na kuwa mbali na vituo walivyojiandikisha jambo ambalo kwa pamoja wameiomba tume ya Taifa ya uchaguzi kuliangalia kwa jicho la pili na hatimaye waweze kuwasaidia wanafunzi hao kutimiza haki hiyo msingi ya kikatiba.
0 comments:
Post a Comment