Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Paul Makonda (katikati), akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari Dar es Salaam leo asubuhi, wakati akipokea msaada wa vifaa vya ujenzi kutoka Mfuko wa GSM ambao pia walitoa magodoro na ahadi ya kuchimba visima 20 vya maji kwa ajili ya kusaidia wilaya hiyo. Kulia ni Mwakilishi wa kampuni hiyo, Elibariki Lukumay na kushoto ni Mkurugenzi Msaidizi wa mfuko huo, Feisal Saleh.
Mkurugenzi Msaidizi wa mfuko huo, Feisal Saleh (kushoto), akizungumza katika mkutano huo.
Mwakilishi wa kampuni hiyo, Elibariki Lukumay (kulia), akizungumza wakati wa kukabidhi msaada huo.
Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Paul Makonda (katikati) akipeana mkono na viongozi wa mfuko huo baada ya kupokea msaada huo.
Wapiga picha wakiwa tayari kuchukua tukio hilo.
Wapiga picha wakiwa kazini.
Mwanahabari Bakari Kahango akiuliza swali katika mkutano huo.
Na Dotto Mwaibale
MFUKO wa GSM umemkabidhi, Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Paul Makonda vifaa vya ujenzi kwa ajili ya kusaidia shule mbalimbali wilayani humo na wananchi.
Akizungumza jijini Dar es Salaam leo wakati wa kukabidhi msaada huo, Muwakilishi wa mfuko huo, Elibariki Lukumay alisema wametoa vifaa hivyo ili kuunga mkono jitihada za mkuu huyo wa wilaya Paul Makonda za kuwaletea maendeleo wananchi wa wilaya yake hasa katika sekta ya elimu.
Lukumay alisema kwamba mfuko wao umetoa madawati 3,000 kwa ajili ya kukabiliana na uhaba wa madawati katika shule za msingi na sekondari katika wilaya hiyo.
Alitaja vitu vingine walivyotoa ni magodoro 500 kwa ajili ya hospitali za wilaya hiyo kufuatia wagonjwa kulala chini na pia wametoa mifuko 1,000 ya saruji, mabati 1000 kwa ajili ya ujenzi wa shule saba ambazo ujenzi wake unaendelea.
Lukumay alisema mbali ya misaada hiyo pia watachimba visima 20, ambapo Makonda ndiye atakayetoa maelekezo ya wapi visima hivyo vichimbwe.
Mkuu huyo wa wilaya hiyo, Paul Makonda aliushukuru mfuko huo kwa msaada huo kwa kumuunga mkono Rais Dk.John Pombe Magufuli za kutoa elimu bure kwa wananchi ambapo aliyataka makampuni na taasisi zingine kuiunga serikali mkono katika suala hilo ili kuwasaidia wananchi na wanafunzi kwa ujumla ili kuhakikisha wanapata mazingira bora ya kupata elimu.
Alisema msaada huo utatoa fursa ya wanafunzi kupata huduma ya maji, madawati na hospitali zitapata magodoro.
0 comments:
Post a Comment