NACTE YAFUNGUA MFUMO WA UDAHILI WA PAMOJA KWA MWAKA WA MASOMO 2016/2017



Kaimu Katibu Mkuu wa  Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi (NACTE) Dk. Adolf Rutayuga, (Kulia) akisisitiza jambo wakati alipokuwa ikitangaza wa kuzindua Mfumo wa Udahili wa Pamoja (Central Admission System (CAS)) kwa mafunzo yanayoratibiwa na Baraza kwa mwaka wa masomo wa 2016/17. Mfumu huo, utatumika kuratibu maombi ya kujiunga na mafunzo ya Astashahada (Cheti), Stashahada (Diploma) na Shahada ya kwanza (“Bachelor Degree)   Katikati ni Mkurugenzi Udhibiti Ubora Rasmalimali watu , Edmund Kinwasi na Kaimu Mkurugenzi  Idara ya  Ufuatiliaji  Tathimini na Uthibiti wa baraza hilo , Christina Kumwenda. Uzinduzi huo ulifanyika leo jijini Dar es Salaam.
 Kaimu Katibu Mkuu wa  Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi (NACTE) Dk .Adolf Rutayuga,  akipofya kitufe cha komputa  kuashiria Uzinduzi  rasmi wa Mfumo wa Udahili wa Pamoja (Central Admission System (CAS)) kwa mafunzo yanayoratibiwa na Baraza kwa mwaka wa masomo wa 2016/17. Mfumu huo, utatumika kuratibu maombi ya kujiunga na mafunzo ya Astashahada (Cheti), Stashahada (Diploma) na Shahada ya kwanza (“Bachelor Degree)  wanaoshuhudia kutoka kulia ni Kaimu Mkurugenzi  Idara ya  Ufuatiliaji  ,Tathimini na Uthibiti ,Christina Kumwenda,  Mkurugenzi  udhibiti  ubora  rasmalimali watu Edmund Kinwas, Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Vyuo ushauri na Mipango Alfred Kilasi,Mkurugenzi Mafunzo na Upimaji Bakari Issa (kushoto) na  Afisa Mifumo ya Kompyuta wa baraza hilo , Daud Mabena.Uzinduzi huo umefanyika leo jijini Dar es Salaam.

 Kaimu Katibu Mkuu wa  Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi (NACTE) Dkt .Adolf Rutayuga(Kushoto) akifafanua jambo  kwa waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam ( hawapo pichani) kuhusiana na Uzinduzi  wa Mfumo wa Udahili wa Pamoja (Central Admission System (CAS)) kwa mafunzo yanayoratibiwa na Baraza kwa mwaka wa masomo wa 2016/17. Mfumu huo utatumika kuratibu maombi ya kujiunga na mafunzo ya Astashahada (Cheti), Stashahada (Diploma) na Shahada ya kwanza (“Bachelor Degree)    wapili kushoto ni   Mkuu wa Kitengo cha Udahili Seremani Majindo, Mkurugenzi wa Mfumo na Upimaji,Bakari Issa  na  Kaimu Mkurugenzi Idara ya vyuo na ushauri na Mipango.Uzinduzi huo ulifanyika leo jijini Dar es Salaam 

BARAZA la Taifa la Elimu ya Ufundi (NACTE), limetangaza ufunguzi rasmi wa Mfumo wa Udahili wa Pamoja (Central Admission System (CAS)) kwa mafunzo yanayoratibiwa na Baraza kwa mwaka wa masomo wa 2016/17. Mfumu huo, utatumika kuratibu maombi ya kujiunga na mafunzo ya Astashahada (Cheti), Stashahada (Diploma) na Shahada ya kwanza (“Bachelor Degree”).

Akizungumza na Waandishi wa Habari jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi wa Maelekezo na Msaada kwa Taasisi wa NACTE, Dk. Adolf Rutayuga amesema kuwa, kwa mwaka wa masomo wa 2015/16, Baraza liliratibu udahili wa wanafunzi katika vyuo mbali mbali kwa kozi za astashahada (Cheti) na stashahada (Diploma) kwa mafunzo ya afya na ualimu yaliyoidhinishwa na Baraza. ameongeza kuwa, Baraza pia  lilishirikiana na Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania, kuratibu udahili wa wanafunzi katika vyuo mbali mbali kwa kozi za shahada ya kwanza kupitia Mfumo wa Udahili wa Pamoja (Central Admission System (CAS)).

“Mifumo hii miwili ilifanyika kwa ufanisi mkubwa na uliwawezesha  waombaji kudahiliwa. Mifumo hii ya udahili imekuwa na mafanikio yafuatayo: Kudhibiti udanganyifu katika udahili uliotokana na baadhi ya waombaji kutumia vyeti vya bandia, kuwapunguzia waombaji gharama za kuomba udahili katika vyuo mbalimbali, kuondoa uwezekano wa mwombaji udahili mmoja kudahiliwa zaidi ya mara moja na kuwanyima waombaji wengine nafasi, kuiwezesha serikali kuwa na takwimu sahihi za waombaji udahili kwa ajili ya kufanikisha mipango ya elimu nchini, na kuwawezesha waombaji udahili kujiunga na mafunzo kwenye taasisi zinazotambuliwa na Serikali,” alieleza.

Dk Rutayuga alieleza kuwa, kwa kutambua mafanikio ya udahili wa pamoja  yaliyopatikana,  Serikali ya kupitia Wizara ya Elimu, Sayansi, Teknolojia na Mafunzo ya Ufundi, imeamua kuwa maombi yote ya udahili kwa ajili ya mafunzo ya Astashahada (Cheti), Stashahada (Diploma) na Shahada ya kwanza (Bachelor Degree) yafanywe kupitia kwenye Mfumo wa Pamoja wa Udahili (CAS). 

Amefafanua kwamba. Baraza linautangazia umma kuwa, kuanzia mwaka wa masomo 2016/2017 udahili wa kozi zote nchini utafanywa kupitia Mfumo wa Udahili wa Pamoja (CAS) unaosimamiwa na NACTE, Vyuo Vikuu  na taasisi za Elimu zote nchini Tanzania zinazotoa mafunzo ya Cheti na Diploma kutodahili wanafunzi nje ya mfumo wa udahili wa Pamoja kuanzia mwaka wa masomo 2016/17.

“Tunapenda kutoa taarifa pia kuwa, maombi ya kujiunga na kozi za Cheti na Diploma yataanza kupokelewa rasmi kupitia Mfumo wa Udahili wa Pamoja kuanzia tarehe 4 Machi 2016, saa sita mchana. Baraza pia litaanza kupokea rasmi maombi ya kujiunga na kozi za Shahada (Degree) kwa wahitimu wenye Diploma kupitia Mfumo wa Udahili wa Pamoja kuanzia tarehe 4 Machi 2016, saa sita mchana,” 

Kwa maelezo zaidi ya jinsi ya kuomba mafunzo kwa kutumia Mfumo wa Pamoja wa Udahili (CAS), alisema Baraza linashauri waombaji watembelee tovuti ya Baraza ambayo ni www.nacte.go.tz.
SHARE
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment