JESHI LA POLISI LASHIRIKIANA NA VODACOM TANZANIA KUTOA MSAADA WA VYAKULA MBALIMBALI KWA KITUO CHA WATOTO YATIMA


Mfanyakazi wa Vodacom Tanzania,Candida Ngido (kushoto) akiongea na Kurwa Simon (kulia)ambaye ni mwanafunzi wa darasa la(7)katika shule ya msingi Muongozo ya Kinondoni jijini Dar es Salaam anayelelewa katika kituo cha watoto wanaishi katika mazingira magumu cha Malaika,wakati wafanyakazi wa kampuni hiyo kwa kushirikiana na jeshi la polisi walipotembelea kituo hicho na kutoa msaada wa vyakula mbalimbali katika mwelendelezo wa kusherehekea siku ya wanawake duniani,katikati ni Dotto Simon.
Mrakibu wa Polisi dawati la jinsia Kinondoni jijini Dar es Salaam, Leah Shindano (kushoto) akimshuhudia Abdallah Rashid (wapili kushoto)ambaye ni mtoto anayeishi katika mazingira magumu na kulelewa katika kituo cha Malaika cha Kinondoni,akipokea msaada wa mfuko wa mchele kwa niaba ya watoto wenzake kituoni hapo toka kwa Mkuu wa kitengo cha Vodacom Foundation, Renatus Rwehikiza (kulia) ikiwa ni msaada uliotolewa na wafanyakazi wa Vodacom Tanzania kwa kushirikiana na jeshi la Polisi katika mwendelezo wa kusherehekea siku ya wanawake duniani.
Abdallah Rashid (watano kushoto) ambaye ni mtoto anayeishi katika mazingira magumu na kulelewa katika kituo cha Malaika cha Kinondoni jijini Dar es Salaam,akipokea msaada wa mfuko wa mchele kwa niaba ya watoto wenzake kituoni hapo toka kwa Mfanyakazi wa Vodacom Tanzania,Glory Njau (kulia) ikiwa ni msaada uliotolewa na wafanyakazi wa kampuni hiyo kwa kushirikiana na jeshi la Polisi katika mwelendelezo wa kusherehekea siku ya wanawake duniani.
Mlezi wa kituo cha kulelea watoto wanaoishi katika mazingira magumu cha Malaika Kinondoni jijini Dar es Salaam,Najma Manji (kulia) akiongea na baadhi ya wafanyakazi wa Vodacom Tanzania walipotembelea kituo hicho kwa kushirikiana na jeshi la polisi kutoa msaada wa vyakula mbalimbali na mafuta ya kula ikiwa ni mwendelezo wa kusherehekea siku ya wanawake duniani,wapili kulia ni Mrakibu wa Polisi dawati la jinsia Kinondoni jijini Dar es Salaam,Leah Shindano.
Mlezi wa kituo cha kulelea watoto wanaoishi katika mazingira magumu cha Malaika Kinondoni jijini Dar es Salaam,Najma Manji (watatu kulia) akipokea msaada wa ndoo ya mafuta ya kula kwa niaba ya watoto wanaolelewa kituoni hapo toka kwa mfanyakazi wa Vodacom Tanzania, Alice Luis(kulia) msaada huo pamoja na vyakula mbalimbali vilitolewa na wafanyakazi wa kampuni hiyo kwa kushirikiana na jeshi la polisi ikiwa ni mwendelezo wa kusherehekea siku ya wanawake duniani,wanne kushoto ni Mrakibu wa Polisi dawati la jinsia Kinondoni,Prisca Komba.
SHARE
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment