Meza
kuu kwenye uzinduzi wa kambi ya upimaji afya kwa watoto walio na umri
chini ya miaka mitano iliyofadhiliwa na Umoja wa Watu kutoka Bengali,
India wanaoishi Tanzania (Bango Sangho) katika shule ya Msingi Kibugumo
iliyopo Kigamboni jana jijini Dar es Salaam. Kutoka kushoto ni Mratibu
wa kambi hiyo ya upimaji kutoka Kliniki ya Al Hilal, Dk.Ali Mzige,
Mwenyekiti wa Umoja wa Jamii ya watu kutoka India, Bengali waliopo
Tanzania (Bango Sangho), Kunal Banerjee, Mwalimu Mkuu wa Shule ya msingi
Kibugumo, Mzamilo Ally, Mgeni rasmi Mkuu wa Wilaya ya Temeke, Sophia
Mjema pamoja na Mbunge wa Jimbo la Kigamboni, Dk. Faustine Ndungulile.
(Picha na Zainul Mzige).
Umoja
wa Watu kutoka Bengali, India wanaoishi nchini (Bango Sangho) umetoa
msaada wa kompyuta, printa, tanki la maji la lita 5000, umeme, madarasa
saba yaliyofanyiwa ukarabati, madaftari na kalamu katika Shule ya Msingi
Kibugumo iliyopo Kigamboni ulio na thamani ya shilingi Milioni 20
pamoja na huduma ya kupima afya kwa watoto walio na umri chini ya miaka
mitano.
Akizungumzia
msaada huo, Mwenyekiti wa Bango Sangho, Kunal Banerjee alisema wameamua
kutoa msaada huo kwa shule ya Msingi Kibugumo na huduma ya kupima bure
kwa kutambua umuhimu wa afya na elimu bora kwa maendeleo ya sasa na
baadae kwa taifa.
Alisema
wamekuwa wakitoa misaada katika shule hiyo kwa mwaka wa tatu mfululizo
na mwaka huu waliamua kuwaletea tena na huduma ya upimaji afya bure kwa
watoto walio na umri chini ya miaka mitano ili wazazi wapate fursa ya
kutambua hali ya afya za watoto wao lakini pia kuwajengea utaratibu wa
kuwapeleka watoto wao katika vituo vya afya ili kujua hali zao za
kiafya.
“Sisi
tunapenda kuona hali nzuri ya elimu na tumeshasaidia kwa muda shule hii
tumeshatoa madawati 100 na tulijenga madarasa mawili na leo tumeleta
msaada mwingine na pia awamu hii tena tumeleta huduma ya afya ili watoto
wapimwe afya zao,” alisema Banerjee.
Mwenyekiti wa Bango Sangho, Kunal Banerjee akisoma risala ya Umoja huo
mbele ya mgeni rasmi Mkuu wa Wilaya ya Temeke, Sophia Mjema na Mbunge wa
Jimbo la Kigamboni, Dk. Faustine Ndungulile.
Nae
mgeni rasmi katika halfa hiyo ya kupokea msaada kutoka Bango Sangho,
Mkuu wa Wilaya ya Temeke, Bi. Sophia Mjema aliwashukuru Bango Sangho kwa
msaada huo ambao wameotoa katika shule hiyo na huduma ya kupima afya
kwa watoto walio na umri chini ya miaka mitano na kuwaomba kama
ikiwezekana wawapelekee huduma hiyo ya kupima afya kila baada ya miezi
mitatu.
Alisema
wilaya yake bado ina changamoto nyingi katika sekta ya elimu na kupitia
msaada huo utaweza kusaidia kuboresha elimu kwa wanafunzi wa shule hiyo
na kuwaomba kuendelea kuwasaidia.
“Wilaya
yetu bado ina changamoto nyingi na kwa msaada huuu naomba niwashukuru
sana na ninaomba muendelee kuwa na moyo huo,” alisema Bi. Mjema.
Aidha
Bi. Mjema aliwataka wananchi wa wilaya yake ya Temeke kuwa na utaratibu
wa kupima afya zao angalau mara moja kwa mwaka ili waweze kutambua
magonjwa waliyonayo kabla hayajaanza kuwasumbua na hata wengine
kupelekea kupoteza maisha kutokana na kutokuwa na utaratibu wa kupima
hadi wanapoanza kusumbuliwa.
Nae
Mratibu wa kambi ya upimaji, Dkt. Ali Mzige alisema kupitia huduma hiyo
ya upimaji wa afya kwa watoto walio na umri chini ya miaka mitano
wanataraji kupima watoto sio chini ya 400 na huduma zitakazotolewa ni
kupima uzito, wingi wa damu, ushauri kuhusu lishe, afya ya kinywa na
watoto watakaobainuka kuwa na matatizo watapewa rufaa kupelekwa
Hospitali ya Wilaya ya Temeke.
Alisema
kupitia huduma hiyo wataweza kutambua magonjwa waliyonayo watoto lakini
pia kuwapa elimu wazazi jinsi ya kuwalea watoto katika mfumo bora wa
kiafya.
“Tunafanya
huduma hii kwa watoto sababu asilimia 32 ya watoto nchini walio na umri
chini ya miaka mitano wamedumaa na pia tutaweza kuwapa vipeperushi
wazazi ili wajue jinsi ya kulea watoto na wanapougua wajue nini cha
kufanya,” alisema Dkt. Mzige.
Nae
mwalimu wa afya katka shule ya Kibugumo, Tatu Mhina aliwashukuru Bango
Sangho kwa misaada ambayo wamekuwa wakiwapatia tangu mwaka 2014 mpaka
sasa na kuwaomba kuendelea na moyo huo wa kusaidia elimu katika shule
hiyo na kuzidi kuwapelekea huduma za kiafya katika jamii inayozunguka
shule hiyo ili wanafunzi waweze kuwa na afya njema.
Mbunge
wa Jimbo la Kigamboni, Dk. Faustine Ndungulile akisisitiza jambo kwenye
uzinduzi huo kabla ya kumkaribisha Mkuu wa Wilaya ya Temeke, Sophia
Mjema kutoa nasaha katika ufunguzi wa kambi hiyo.
Mkuu
wa Wilaya ya Temeke, Sophia Mjema akitoa neno la ufunguzi wa kambi ya
upimaji afya kwa watoto wenye umri chini ya miaka mitano iliyofadhiliwa
na Umoja wa Watu kutoka Bengali, India wanaoishi Tanzania (Bango Sangho)
katika shule ya Msingi Kibugumo iliyopo Kigamboni jana jijini Dar es
Salaam.
Mkuu
wa Wilaya ya Temeke, Sophia Mjema (katikati) akimpima uzito mtoto
Shafii Haji (mwaka mmoja na nusu) mkazi wa Kibugumo Darajani, kama
ishara ya kuzindua kambi ya huduma za upimaji afya kwa watoto walio na
umri chini ya miaka mitano iliyofadhiliwa na Umoja wa Watu kutoka
Bengali, India wanaoishi Tanzania (Bango Sangho) katika shule ya Msingi
Kibugumo iliyopo Kigamboni jana jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Mratibu
wa kambi hiyo kutoka Kliniki ya Al Hilal, Dk. Ali Mzige, Mbunge wa
Jimbo la Kigamboni, Dk. Faustine Ndungulile (wa kwanza kulia) pamoja na
Muuguzi wa Zahanati ya Kibugumo, Agnes Mokiwa (wa pili kulia)
wakishuhudia tukio hilo.
Mkuu
wa Wilaya ya Temeke, Sophia Mjema (katikati) akiwa amembeba mtoto
Shafii Haji (mwaka mmoja na nusu) mkazi wa Kibugumo Darajani, baada
zoezi la kumpima uzito wakati akizindua kambi ya huduma za upimaji afya
kwa watoto walio na umri chini ya miaka mitano iliyofadhiliwa na Umoja
wa Watu kutoka Bengali, India wanaoishi Tanzania (Bango Sangho) katika
shule ya Msingi Kibugumo iliyopo Kigamboni jana jijini Dar es Salaam.
Mkuu
wa Wilaya ya Temeke, Sophia Mjema akikagua kadi ya kliniki ya maendeleo
ya mtoto Shafii Haji (mwaka mmoja na nusu) mkazi wa Kibugumo Darajani
(hayupo pichani) mara baada ya kuzindua kambi ya upimaji afya kwa watoto
walio na umri chini ya miaka mitano iliyofadhiliwa na Umoja wa Watu
kutoka Bengali, India wanaoishi Tanzania (Bango Sangho) katika shule ya
Msingi Kibugumo iliyopo Kigamboni jana jijini Dar es Salaam. Kushoto ni
Mratibu wa kambi hiyo kutoka Kliniki ya Al Hilal, Dk.Ali Mzige na Kulia
ni Muuguzi wa Zahanati ya Kibugumo, Agnes Mokiwa.
Wanafunzi
wa Shule ya Msingi Kibugumo iliyopo Kigamboni jijini Dar es Salaam
wakigaiwa madaftari yaliyotolewa kama zawadi na Umoja wa Watu kutoka
Bengali, India wanaoishi Tanzania (Bango Sangho).
Mkuu wa Wilaya ya Temeke, Sophia Mjema akielekea kuzindua moja ya madarasa yaliyokaribatiwa na kuwekewa umeme na Bango Sangho.
Mkuu
wa Wilaya ya Temeke, Sophia Mjema akikata utepe kuzindua moja kati ya
madarasa yaliyokarabatiwa na Bango Sangho huku Mwenyekiti wa Bango
Sangho, Kunal Banerjee (kushoto) na Mbunge wa Jimbo la Kigamboni, Dk.
Faustine Ndungulile wakishuhudia tukio hilo.
Muonekano
wa vyumba vya madarasa katika shule ya Msingi Kibugumo baada ya kupakwa
rangi na kuwekwa umeme na Umoja wa Watu kutoka Bengali, India wanaoishi
Tanzania (Bango Sangho).
Mkuu wa Wilaya ya Temeke, Sophia Mjema akikagua moja ya darasa lililokarabatiwa na Bango Sangho.
0 comments:
Post a Comment