MAUZA UZA SHULE YA MSINGI MHANGA WANAFUNZI WAANGUKA OVYO CHANZO VIJITI

Mbunge wa Kilolo Venance  Mwamoto  akizungumza na  wanafunzi wa  shule ya Msingi Mhanga ambao wameumbwa na ugonjwa wa kuanguka.

Mbunge  Mwamoto akiwa na  walimu ,wanafunzi na viongozi wa chama na serikali ngazi ya wilaya  na mkoa
Mbunge  Mwamoto  akiwa na  walimu wa  shule   hiyo
Walimu  wa  shule ya Msingi Mhanga  wakiwa katika  hali ya  hofu  
---
WANAFUNZI  wa shule ya Msingi Mhanga  kata ya  Kimara  wilaya ya Kilolo wakumbwa na ugonjwa  wa  kuanguka ovyo kwa  zaidi ya miezi sita sasa chanzo kikitajwa  kuwa ni  vijiti vya ajabu  vilivyokutwa  mfukoni mwa  mwanafunzi mmoja msichana anayesoma  darasa  la saba .

Mwalimu mkuu wa  shule   hiyo  Zamoyoni Mvella  akitoa  taarifa  ya  kuanguka kwa  wanafunzi hao mbele ya  mbunge  wa  Kilolo Bw Venance Mwamoto  jana  alisema  kuwa  tatizo hilo la  wanafunzi  kuanguka  limekuwa  likijitokeza kila  siku kwa  zaidio ya  miezi 6  sasa mfululizo na  kuwa idadi ya  siku moja kwa wanafunzi  kuanguka ni kati ya 8 hadi  wanafunzi 16 kwa  siku .

Alisema kuwa tatizo hilo  lilianza kwa  mwanafunzi mmoja  wa darasa la  saba   aliyemaliza mwaka  jana ila kwa  sasa  limeendelea  kwa  kasi  kutoka mtoto  mmoja  hadi  kufikia watoto zaidi ya 15 kwa  siku  mmoja .

Mkuu  huyo  alisema  kuwa wanafunzi   wanaoongoza  kuanguka  zaidi na  wasichana  huku wavulana ni mtoto  mmoja  pekee na  kuwa  jitihada za uongozi wa  shule  hiyo ambazo zimefanyika  ni pamoja na  kutoa  taarifa  kwa viongozi wa  elimu ngazi ya juu  ikiwa  ni pamoja na  kuwaita wazazi wote  wa  wananfunzi  wanaosoma  katika  shule  hiyo  wakiwemo  viongozi wa  dini zote .

Hata  hivyo  alisema  kutokana  na kasi  hiyo  ya  wanafunzi  kuanguka  kuwa  juu hofu  imezidi  kutanda  hadi kwa  walimu ambao wamekuwa  wakihofu kuendelea   kufundisha  shule   hiyo kutokana na ugonjwa  huo  kutishia maisha  yao.

Mwenyekiti  wa serikali ya kijiji hicho Bw. Emelius Kihongosi alisema   kuwa wanafunzi hao   wamekuwa  wakianguka  kama  wagonjwa wa  kifafa ila  baada ya  kufanya  tafiti  imebainika  kuwa  wanafunzi hao  hawana ugonjwa  wa  kifafa  ila  wanasumbuliwa na pepo .

Alisema  kuwa chanzo  cha tatizo hilo ni  mwanafunzi mmoja  msichana  wa darasa la saba aliyeanguka  na baada ya  kuzinduka   alikuta  vijiti mfukoni mwake na baada ya  kukuta  vijiti  hivyo aliwaonyesha  wenzake ambao mmoja aliyevitazama pia alianguka na  yule aliyetaka  kuvichukua vijiti hivyo  ili  kuvitupa naye  pia  alianguka pia  wakati wanafunzi  wakishangaa kwa  kutaka  kuteketeza  vijiti hivyo  vya ajabu ndipo alitokea mtu  wa ajabu aliyevalia nguo vyeupe  na  kuchukua  vijiti  hivyo na  kutoweka navyo porini.</td></tr>
</tbody></table>


SHARE
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment