Meneja wa huduma za jamii wa Airtel, Hawa Bayumi (Kulia) akizungumza
na vyombo vya habari wakati wa hafla ya makabidhiano ya kompyuta 30 kwa
Chuo cha Taifa cha Utalii (NCT) kwa kupitia mpango wa Airtel FURSA ili
kuwawezesha wanafunzi kujifunza elimu ya ujasiriamali kwa njia ya
kisasa, akishuhudiwa na Meneja Msaidizi wa chuo Oscar Mwambene
(katikati) pamoja na Mkurugenzi wa Mafunzo Eunice Nderingo Ulomi
(kushoto), hafla hiyo ilifanyika chuoni hapo Temeke, Dar es Salaam.
Mkuu wa idara ya Utalii katika Chuo cha Taifa cha Utalii Elina
Makanja (Kushoto) akimwelekeza mwanafunzi Agape Gerald (Kulia) mara
baada ya kukabidhiwa kompyuta 30 kwa kupitia mpango wa Airtel FURSA ili
kuwawezesha wanafunzi kujifunza elimu ya ujasiriamali kwa njia ya
kisasa, akishuhudiwa na Meneja wa huduma za jamii wa Airtel, Hawa Bayumi
(Katikati)
Meneja wa huduma za jamii wa Airtel, Hawa Bayumi (kushoto)
akizungumza na Mkurugenzi wa Mafunzo Eunice Nderingo Ulomi (kulia)
pamoja na Mkuu wa idara ya Utalii Elina Makanja (katikati) wakati wa
hafla ya makabidhiano ya computer 30 kwa Chuo cha Taifa cha Utalii (NCT)
kwa kupitia mpango wa Airtel FURSA ili kuwawezesha wanafunzi kujifunza
elimu ya ujasiriamali kwa njia ya kisasa.
Baadhi
ya wanafunzi wa chuo cha Taifa cha Utalii (NCT) wakitumia kompyuta
zilizokabidhiwa na Airtel kwa kupitia mpango wa Airtel FURSA ili
kuwawezesha kujifunza elimu ya ujasiriamali kwa njia ya kisasa.
---
Katika
kuendeleza dhamira yake ya kusaidia Jamii kwa kujenga ubora wa ya
elimu ya ICT hapa nchini, Airtel imekabidhi kompyuta 30 kwa Chuo cha
utalii cha Taifa (NCT) ambapo ni sehemu mojawapo ya mipango yake ya
kusaidia vijana wajasiriamali hapa nchini ujulikanao kama Airtel FURSA
wa kutoa huduma kwa jamii katika kuboresha upatikanaji wa teknolojia ya
kisasa na ubora wa elimu nchini Tanzania.
Kama kampuni
yenye kutoa huduma bora za simu za mkononi, Airtel itaendelea kusaidia
sekta ya ICT hapa nchini kwa kuwawezesha vijana kupata elimu iliyobora
na kuwa vijana wenye mafanikio katika Jamii yao.
Akizungumza
wakati wa sherehe za makabidhiano hayo yaliyofanyika katika Chuo cha
utalii cha Taifa (NCT) kilichopo Temeke, meneja huduma kwa jamii wa
Airtel, Hawa Bayumi alisema kuwa Airtel itaendeleza dhamira yake ya
kuunga mkono juhudi ya kuboresha kiwango cha elimu hapa nchini.
“
Leo hii tumekabidhi kompyuta hizi tukiamini kwamba tunachangia nchi
yetu kuwa na elimu bora, ni jambo la muhimu kwa wanafunzi na walimu kuwa
na vifaa bora mashuleni. Ndio maana Airtel imeweka mkazo katika swala
la kusaidia Jamii kwa upande wa elimu kwa kutoa vitendea kazi
vitakavyoweza kusaidia kujifunzia na kupata elimu ya ujasiriamali na
hatimaye kuchangia vyema na kupata matokeo bora. Kutokana na msaada huu
kwa NCT tunaamini kabisa kwamba kiwango cha elimu kwa Wanafunzi
kitaongezeka na hata urahisi wa walimu katika ufundishaji utaongezeka
kwa kiwago kikubwa, na vile vile tunawawezesha kizazi kijacho kujikita
zaidi katika teknolojia na kujua mambo mengi zaidi yanayoendelea dunia
nzima kutokana na technolojia inayokuwa kila siku, "alisema Bayumi.
Akizungumza
kwa niaba ya chuo, mkurugenzi wa Mafunzo wa NCT, Eunice Nderingo Ulomi,
aliwashukuru Airtel kwa kwa msaada huo wa kompyuta , na kubainisha kuwa
kompyuta hizo zitachangia kuongeza kiwango cha elimu kwa mwanafunzi
kitaaluma. "Mara nyingi kompyuta huwa inatazamwa kama si kitu cha muhimu
katika Jamii yetu, ila ni kifaa muhimu sana kinachomuwezesha mwanafunzi
kupata habari nyingi sana za masomo na hata kujua mambo mbalimbali
yanayoendelea dunia nzima hasa katika karne hii ya 21," alisema Ulomi.
"Lengo
letu ni kuhakikisha tunatoa elimu iliyobora katika sekta ya utalii .
Kupokea kompyuta hizi kutaboresha hali ngumu tuliyakuwanayo ya upungufu
wa vifaa hivi hapa chuoni na tunaamini tutatoa elimu iliyobora ambayo
itasidia kupunguza changamoto tulizakuwanazo, ambazo zimekuwa
zikitufanya tukwame katika mambo mengi sana, hivyo zitatusaidia kukuza
ujuzi wa kila mtu hapa chuoni, vile vile zitasaidia kuongeza mapato ya
serikali, kukuza nchi yetu katika ushindani wa kitalii na kuongeza
uingizaji wa watalii ambapo itasaidia kuongeza sekta nyingine za
kiuchumi katika upande wa maonyesho ", aliongeza Ulomi.
0 comments:
Post a Comment