Wanafunzi wa Chuo Cha RUCU walianzisha mgomo wa kutoingia madarasani, kushinikiza bodi ya mkopo kuwapatia pesa zao za awamu ya nne kwa mwaka wa masomo 2014/2015.
Kwa mujibu wa chanzo chetu cha habari kimesema kuwa walitakiwa kupewa pesa zao kuanzia tarehe 3 mwezi huu na mpaka sasa hakuna dalili zozote za hata kusaini.
Chanzo hicho kilisema kuwa mgomo ulianzia saa 3 asubuhi hadi saa 7 mchana kwa wanafunzi kutoingia madarasani hadi mkuu wa chuo alipotuliza kunji hilo.
"Principle wa chuo ndiye aliyekuja kuokoa jahazi, kutokana na ahadi yake aliyoitoa mbele yetu akitutaka tuwasubili walioenda Dar es salaam watuletee majibu ninini kinachochelewesha pesa zetu.
Na sisi tumemkubalia kwa busara zetu na kwa heshima kwake lakini tunataka majibu ya kweli kutoka huko bodi ya mikopo na si siasa" Alisema mwanafunzi huyo.
Akiongea na wanafunzi, mkuu wa chuo, aliwataka wanafunzi kuwa wavumilivu, kwakuwa viongozi wao wa serikali ya wanafunzi wameenda Makao makuu ya bodi ya mikopo, Dar es salam kufuatilia suala hilohilo.
Kwa upande wake Waziri wa mikopo wa serikali ya wanafunzi ya RUCU, Rajabu Bashiri, baada ya kuongea na mwandishi wetu alisema kuwa, wanafunzi waliwabandikiwa tangazo kuwa wawe na subira kidogo kwakuwa tatizo hilo linashugulikiwa kwa sasa kwa bahati mbaya akiwa Dar es salaam ndio akaambiwa kuwa wanafunzi wameanza mgomo.
"Kwa sasa niko Dar es salaam na kufuatilia masuala hayo hayo ya boom na kwa bahati mbaya au nzuri mgomo ulitokea baada ya mimi kuondoka kuja Dar es salaam, na mimi nilipewa taarifa tu." Alisema Rajabu.
Mlolongo wa malalamiko ya boom kwa vyuo vikuu Tanzania umeendelea kushika kasi kila kona kutokana na bodi ya mikopo kuwacheleweshea wanafunzi pesa zao za awamu ya nne kwa mwaka wa masomo 2014/2015.
0 comments:
Post a Comment