Baadhi ya Wanafunzi wakiwa Darasani.
Baadhi ya wanafunzi wakijifunza kushona.
Masomo yakiendelea kwa baadhi ya wanafunzi.
TAASISI ya Don Bosco Net Tanzania yahamasisha
wasichana katika kujiendeleza kimapato na kimawazo kutokana na wasichana wengi
baada ya kumaliza elimu ya Msingi au Sekondari kutofanikiwa
kuendelea na masomo yao ya juu kwasababu mbali mbali. Moja wapo ikiwa ada, hali
ngumu ya uchumi na maisha inayositisha ndoto yao yakujimudu na kujiendeleza.
Taasisi hiyo imeaanda Kampeni ya uhamasishaji kwa
ajili ya wasichana katika Mikoa ya Dar es Salaam na Dodoma kuwahimiza wasichana
wapende na kushiriki mafunzo ya ufundi stadi yatolewayo na vyuo vya ufundi Don
Bosco- Tanzania.
.
Taasisi hiyo ambayo huwasaidia vijana wa hali ya
chini, inaamini vijana wa kiume na kike wana
uwezo sawa, hivyo inatoa vipaumbele kwa wasichana na imeandaa kampeni
maalum kwa ajili ya wasichana ijulikanayo kama BINTI THAMANI. Kampeni hii
inanuia kumkwamua msichana kiuchumi pamoja na kimawazo.
Taasisi ya Don Bosco Tanzania, inatoa mafunzo
mbalimbali kwa wasichana ambayo ni Ufundi umeme, uchomeleaji vyuma, ufundi
uashi , fundi bomba, uchapishaji, ushonaji ,ufundi magari, ufundi umeme,
Kompyuta na uaziri.
Hayo yamesemwa na Mkurugenzi wa Taasisi ya Don Bosco
Net, Fr. Celestine Kharkongor wakati akizungumza na mwandishi wetu jijini
Dar es Salaam leo katika kituo cha Taasisi hiyo Oysterbay jijini Dar es Salaam.
Nae Afisa Mipango wa Taasisi ya Don Bosco
Net-Tanzania, Rosemary Njoki amewasihi wasichana na jamii kwa ujumla kuwa
wapanue mawazo yao hasa katika jamii hii ya sasa ambapo msichana baada ya
kumaliza masomo ana uwezo mkubwa wa kujifunza na kujiwezesha kiuchumi kupitia
mafunzo haya.
Njoki amesema kuwa wasichana ambao wamekata tamaa ya
maisha na elimu kuwa wanauwezo na nafasi ya kujikwamua tena kupitia kampeni
hii. Sanjali na hayo, anawasihi wasichana wote kutembelea vyuo vyao vya ufundi
vya Don Bosco ilikutimiza azima yao ya kujitegemea.
Zaidi ya masomo ya ufundi, Taasisi Tasisi ya Don Bosco inaitoa masomo mtambuka kama (ujasiria mali,chuo cha maisha , na pia somo la uajiri) ili kumuwezesha msichana kujiajiri au kuajiriwa. Hivyo kila binti ana uwezo wa kusoma, kujihusisha na kujiendeleza.
Zaidi ya masomo ya ufundi, Taasisi Tasisi ya Don Bosco inaitoa masomo mtambuka kama (ujasiria mali,chuo cha maisha , na pia somo la uajiri) ili kumuwezesha msichana kujiajiri au kuajiriwa. Hivyo kila binti ana uwezo wa kusoma, kujihusisha na kujiendeleza.
0 comments:
Post a Comment